Nenda kwa yaliyomo

Real Sociedad

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Real Sociedad
Jina kamiliReal Sociedad de Fútbol Sociedad Anónima Deportiva (S.A.D.)
Jina la utaniLa Real, Weupe na Bluu
Imeanzishwa7 September 1909 (Kama Sociedad de Football de San Sebastian)
UwanjaAnoeta Stadium (Reale Arena)
(Uwezo: 39,500)
KochaImanol Alguacil
LigiLa Liga
Tovuti[realsociedad.eus tovuti ya klabu]
Rangi nyumbani
Rangi za safari

Real Sociedad de Fútbol, maarufu kama Real Sociedad, ni klabu ya mpira wa miguu kutoka Hispania yenye maskani yake katika mji wa San Sebastián, katika eneo la Wabaski. Klabu hii ilianzishwa 7 Septemba 1909 na ni moja kati ya vilabu vya zamani na vyenye historia ndefu katika La Liga.

Real Sociedad inachezea mechi zake za nyumbani katika uwanja wa Reale Arena (maarufu kama Anoeta), wenye uwezo wa kuchukua zaidi ya mashabiki 39,000. Kwa miaka mingi, klabu hii imekuwa na utambulisho wa kuendeleza vipaji vya ndani, hasa kutoka eneo la Basque, ingawa isiku za karibuni, imekuwa ikichukua pia vipaji kutoka maeneo ya nje ya ukanda huo. Baadhi ya vipaji vilivyozalishwa na Real Sociedad ni pamoja na Xabi Alonso, Antoine Griezman na Mikel Oyarzabal.

Moja ya mafanikio makubwa ya Real Sociedad yalikuja mwanzoni mwa miaka ya 1980, ambapo walitwaa mataji mawili ya La Liga mfululizo (1980–81 na 1981–82). Pia wamewahi kushinda Kombe la Mfalme (Copa del Rey) mara mbili, mara ya kwanza mwaka 1909 na mara ya pili mwaka 2020 baada ya kuifunga Athletic Bilbao katika fainali ya Basque Derby.

Real Sociedad na Athletic Bilbao zimekuwa na upinzani wa kihistoria (upinzani wa jadi).

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Real Sociedad kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.