Nenda kwa yaliyomo

Radama II

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Rakoto Radama)
Radama II, mfalme 1861-1863.

Mfalme Radama II wa Wamerina kisiwani Madagaska alitawala miaka miwili tu, kati ya kifo cha mama yake, malkia Ravalona I (1861) na kifo chake mwenyewe (1863).

Shughuli zake zilielekezwa katika kuzibadilisha sera zote zilizokuwa zinapinga mambo yaliyoletwa na Wazungu ambazo mfalme aliyetangulia alikuwa akizitumia. Mwelekeo huo ulisababisha upinzani mkubwa dhidi ya utawala wake kutoka kwa watu mashuhuri nchini humo, hali iliyosababisha kuanguka kwake.

Sera ya mfalme ya kusaini mikataba ya siri bila ya maofisa wake kufahamu iliongeza mashaka zaidi kwa viongozi hao. Zaidi ya hayo, kuongezeka kwa athari za wamisionari na Wazungu wengine kitalani kwa mfalme hakukusaidia kitu.

Jambo lililommaliza kabisa ni jaribio lake la kuwaondoa baadhi ya maafisa waandamizi wa nchi ambao ndio walikuwa uti wa mgongo wa serikali yake na badala yao kuwaweka marafiki wake wa ujanani.

Hili lilifufua mlolongo mrefu wa malalamiko dhidi ya mfalme, na tarehe 12 Mei 1863 akauawa.

Baada yake, watawala walikuwa vibaraka tu wa Wazungu, hadi nchi ilipogeuzwa kuwa koloni la Ufaransa.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Radama II kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.