Nenda kwa yaliyomo

Raiders of the Lost Ark

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Raiders of the Lost Ark ni filamu ya Kimarekani ya mwaka 1981 ya mapigano na matukio ya kusisimua (action-adventure), iliyoongozwa na Steven Spielberg na kuandikwa na Lawrence Kasdan, ikitokana na hadithi ya George Lucas na Philip Kaufman.

Hadithi ya filamu hii imewekwa mwaka 1936 na inamshirikisha Harrison Ford katika nafasi ya Indiana Jones, mwanaakiolojia anayesafiri duniani kote kutafuta hazina na mabaki ya kihistoria. Katika filamu hiyo, Jones anashindana na majeshi ya Ujerumani ya Wanazi katika jitihada za kulipata Sanduku la Agano (Ark of the Covenant), ambalo linaaminika kuwa na uwezo wa kulifanya jeshi lolote lisishindike vitani.[1]

Akiungana na mpenzi wake wa zamani mwenye ujasiri, Marion Ravenwood (aliyechezwa na Karen Allen), Indiana Jones anakimbizana na wakati ili kumzuia mwanaakiolojia mpinzani, René Belloq (aliyechezwa na Paul Freeman), asiwaongoze Wanazi kulipata Sanduku hilo na kutumia nguvu zake za ajabu.

A photograph of a replica of the Ark of the Covenant on display
Nakala ya Sanduku la Agano ikionyeshwa mwaka wa 2016
  1. ↑ "Wendie Malick knows exactly why she wasn't cast in 'Raiders of the Lost Ark'". Entertainment Weekly.