Rafika Chawishe
Rafika Chawishe ni mwanaharakati mahiri wa haki za watoto, mwigizaji wa jukwaani na filamu, na pia yeye ni mkurugenzi wa makala za sanaa ya video na makala ya tamthilia. Kama mwanaharakati, amefanya kazi kubwa kwa watoto wakimbizi wasio na wazazi katika kituo cha kwanza cha mapokezi kilichopo kwenye kisiwa cha Lesvos, Moria nchini Ugiriki.[1]
Kama mwigizaji, ameigiza katika filamu iliyoshinda tuzo ya A. AVRANAS Miss Violence, iliyotayarishwa na Faliro House Productions S.A. Kwa sasa, anaonekana katika filamu ya Dance fight, love die iliyotayarishwa na Asteris Koutoulas kuhussu Mikis Theodorakis, ambapo anacheza jukumu dogo la Melina Merkouri. Filamu hiyo ilichaguliwa kushiriki katika mashindano rasmi la Tamasha la Kimataifa la Filamu la Hoff. Jukwaani, ameigiza sehemu nyingi katika maonyesho ya Ukumbi wa Kitaifa kama vile Tamasha la Athens, ukumbi wa michezo wa kale wa Epidavre n.k. Tunaweza kutaja kwa mifano dhahiri kama vile sehemu ya "Solange" katika tamthilia ya Maids of Jean Genet iliyoongozwa na mkurugenzi mwingereza Bruce Myers, mke myahudi wa B. Brecht iliyoongozwa na F. Papadodima na sehemu ya mwanaume aliyebadili jinsia Eidrian/Fiona kwenye tamthilia ya Rotterdam na Jon Brittain.[2][3][4][5]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ ""Τα παιδιά μιλούν ζωγραφίζοντας- Ας τα ακούσουμε!"". firstreception.gov.gr. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-03-27. Iliwekwa mnamo 2026-01-30.
- ↑ NEWSROOM IEFIMERIDA.GR (2017-12-27). "Η βραβευμένη με Ιψεν, Ραφίκα Σαουίς, σε μία παράσταση για το φύλο και τη σεξουαλικότητα [εικόνες]". iefimerida.gr (kwa Kigiriki). Iliwekwa mnamo 2026-01-30.
- ↑ "H Φιόνα/Έντριαν αγαπάει την Άλις". AthensVoice (kwa Kigiriki). 2017-12-13. Iliwekwa mnamo 2026-01-30.
- ↑ Ηρόστρατος (2018-01-10). "Ραφίκα Σαουίς, ηθοποιός-σκηνοθέτης: Μεγαλώνουμε υπόδουλοι να υπηρετούμε στερεότυπα". Δρόμος της Αριστεράς (kwa Kigiriki). Iliwekwa mnamo 2026-01-30.
- ↑ "«Οι δούλες» του Ζαν Ζενέ - Εθνικό Θέατρο". www.n-t.gr (kwa Kigiriki). Iliwekwa mnamo 2026-01-30.
| Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Rafika Chawishe kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |