Rafiatou Karimou
Rafiatou Karimou (2 Mei 1946 – 4 Januari 2018)[1] alikuwa mwanasiasa na mwalimu wa kitaaluma kutoka Benin. Karimou alikuwa mwanamke wa kwanza kuteuliwa kushika wadhifa wa uwaziri katika nchi yake.
Wasifu
[hariri | hariri chanzo]Rafiatou Karimou alizaliwa mwaka 1946 huko Sakété, kusini mwa eneo la Benin ya sasa, wakati huo likijulikana kama Koloni ya Dahomey. Akiwa bado kijana, alianza kushiriki katika shughuli za kijamii kupitia Umoja Mkuu wa Wanafunzi wa Dahomey (UGEED) kabla ya kujiingiza katika siasa. Mwaka 1975, alikuwa mwanamke wa kwanza kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya nchini Benin, na mwaka 1989 akawa mwanamke wa kwanza kuwa waziri nchini humo baada ya kuteuliwa na Rais Mathieu Kérékou kuwa Waziri wa Afya ya Umma.
Alishikilia wadhifa huu hadi mwaka 1990. Baadaye aliteuliwa tena kuwa waziri kuanzia mwaka 2003 hadi 2006, safari hii akiongoza wizara ya Elimu ya Msingi na Sekondari.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Décès de Karim Rafiatou hier à Paris La première femme ministre du Bénin n'est plus". Iliwekwa mnamo 1 Mei 2018.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Bénin : l'ancienne ministre Rafiatou Karimou est décédée de suite d'une longue maladie". 5 Januari 2018. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-06-11. Iliwekwa mnamo 1 Mei 2018.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Rafiatou Karimou kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |