Rachael Okonkwo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Rachael_Okonkwo

Nnenna Rachael Okonkwo (Alizaliwa mnamo tarehe 26 mwezi Mei Mwaka1987) maarufu kwa jina la Nkoli Nwa Nsukka ni mwigizaji filamu wa kike wa Nigeria.[1]

Maisha na kazi[hariri | hariri chanzo]

Rachael Okonkwo anatokea Ukpata huko Uzo Uwani katika jimbo la Enugu , iliyopoto kusini mashariki mwa Nigeria. Alianza kuigiza akiwa mtoto, lakini kutokana na ukosefu wa uhusika katika filamu, alihamia katika uchezaji wa muziki. Alijiunga katika soko la filamu za Nigeria mwaka 2007 akiwa kama mhusika mdogo. Mwaka 2008, alikua mshiriki msaidizi katika filamu ya Ini Edo & Van Vicker kwa jina la Royal War 2, pia mwaka 2010 akiwa na Patience Ozokwor pamoja na John Okafor katika filamu ya Open and Close 1&2. Uhusika wake mkuu wa kwanza na ndiyo iliyompatia umaarufu ni mwaka 2014, alipokua mhusika mkuu katika filamu ya Nkoli Nwa Nsukka kama Nkoli.[2][3] Mama yake alifariki mwaka 2020.[4]

Shughuli za kibinadamu[hariri | hariri chanzo]

Sherehe ya Watoto ya Pasaka[hariri | hariri chanzo]

Katika njia ya kipekee, Rachael Okonkwo alijitolea kwa jamii yake kwa kuongoza sherehe za pasaka zilizolenga kutoa zawadi za bure kwa Watoto pamoja na burudani kwa watu. Alisema hii ilimsaidia kukutana na mashabiki zake. Mwaka 2015 aliandaa sherehe ya kwanza ya pasaka kwa Watoto akiwa na lengo la kuwapatia zawadi mbalimbali, sherehe hiyo ilifanyika huko Enugu.[5] Mwaka 2016 sherehe ya pili ilifanyika Onitsha, hii ilikua na washiriki wengi zaidi kwani aliambatana na waigizaji wenzake kama Ken Erics.[6] Mwaka 2017 sherehe hizo zilifanyika katika mji wake wa nyumbani Nsukka, alifanikiwa kukusanya watu zaidi ya 5000, alishirikisa wasanii wengi zaidi kama Angela Okorie, Nonso Diobi,Slowdog,Ken Erics,Nani Boi, Eve Esin na aliungwa mkono na mashirika makubwa yaliyopelekea kufanya sherehe kubwa zaidi.[7]

Tuzo[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Tuzo Kipengele Matokeo Maelezo
2016 City People Entertainment Awards".[8] Muigizaji bora mshiriki Alishiriki
2015 Karis Media Awards.[9] Mchekeshaji bora wa mwaka Alishiriki
City People Entertainment Awards [10] Muigizaji bora mshiriki wa mwaka Alishiriki

Sanaa zilizochaguliwa[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Filamu Uhusika Maelezo
2020 Small Chops Uzo
2019 The Ghost and the Tout
Nimbe Mira
2017 Teri Teri
Arthur One Eye Amanda
Onwa Na South
Left Over Mhusika Mkuu Regina Daniels
Zee World Madness Kasarachi wahusika wakuu Eve Esin, Nonso Diobi
2016 University Girls Joy Wahusika wakuu Queen Nwokoye, Eve Esin
Vale of Tears Ola wahusika wakuu Yul Edochie,Chiwetalu Agu
Not My Child Nneka Jnr Mhusika mkuu Walter Anga
Ojawa-Nwa Orjiugo
2015 Justify My Love Mary Mhusika mkuu Tonto Dikeh
Eno my calabar love Peace Mhusika mkuu Ini Edo, Osita Iheme
Ijele the princess of fire Ijele
Local Prostitute Chinwe Mhuysika mkuu Patience Ozokwor
Please leave my husband Mercy Wahusika wakuu Ken Erics, Eve Esin
Tears Of Betrayal Asanwa Mhusika mkuu Diamond Okechi
The Gods Anger Chinwe Wahusika wakuu Patience Ozokwor,
Ogidi Olamma Zack Orji, Ebele Okaro
2014 Bloody War Janet Wahusika wakuu Ken Erics, Ngozi Ezeonu
Paw Paw the guitar boy Ada Wahusika wakuu Osita Iheme, Michael Godson
Nkoli Nwa Nsukka Nkoli
2013 Sister Esther Loveth
2010 Open & Close Anulika Wahusika wakuu John Okafor,Patience Ozokwor
2008 Royal War 2 Amaka Wahusika wakuu THOMPSON, Van Vicker

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Actress Rachael Okonkwo and mother both look young in new photo". Naij. Iliwekwa mnamo 27 April 2017.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "I wont sacrifice my career for marriage - Nollywood Diva Rachael Okonkwo". The Nation Online. Iliwekwa mnamo 27 April 2017.  Check date values in: |accessdate= (help)
  3. "Rachael Okonkwo Biography: Top 5 things you should know". Fab 36. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-11-04. Iliwekwa mnamo 27 April 2017.  Check date values in: |accessdate= (help)
  4. Adene, Gift (30 October 2020). "Bisola Badmus, Destiny Etiko and other celebrities whose parent died in 2020". Kemi Filani News.  Check date values in: |date= (help)
  5. "Rachael Okonkwo Goes Completely Bald In New Photos". Koko Tv. Iliwekwa mnamo 27 April 2017.  Check date values in: |accessdate= (help)
  6. "Photos from actress Rachael okonkwo aka nkoli nwa nsukka easter carnival". Linda Ikeji. Iliwekwa mnamo 27 April 2017.  Check date values in: |accessdate= (help)
  7. "Nkoli nwa nsukka storms nsukka for children's easter carnival". Stella Dimokokokorkus. Iliwekwa mnamo 27 April 2017.  Check date values in: |accessdate= (help)
  8. "City People Entertainment Awards 2016 “Suruler”,”Tinsel”,”Adeniyi Johnson”,Mide Martins among nominees". Pulse Nigeria. Iliwekwa mnamo 27 April 2017.  Check date values in: |accessdate= (help)
  9. "Karis Media Awards.Nominees list for the 2015 edition". Pulse Nigeria. Iliwekwa mnamo 27 April 2017.  Check date values in: |accessdate= (help)
  10. "Awards: Full nominee list of city people awards". Jaguda. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-08-12. Iliwekwa mnamo 27 April 2017.  Check date values in: |accessdate= (help)