Nenda kwa yaliyomo

Rabia Djelti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Rabia Djelti (amezaliwa 1954) ni mwandishi wa Algeria anayejua vizuri lugha za Kiarabu na Kifaransa. Mwaka wa 2002, kwa mchango wake katika ushairi na riwaya, alitunukiwa tuzo ya fasihi ya Kiarabu huko Abu Dhabi.[1] Mbali na uandishi, Djelti anafundisha fasihi katika Chuo Kikuu cha Algiers.[2]

Alizaliwa tarehe 5 mwezi Agosti mwaka wa 1954 katika mji wa Nedroma. Alisoma shule ya msingi ya nchini Morocco kabla ya kuendelea na elimu yake ya sekondari mjini Oran (mwaka wa 1969 hadi mwaka wa 1975).[3] Tangu akiwa mdogo alivutiwa na fasihi ya Kifaransa, aligundua kazi za waandishi kama Baudelaire na Victor Hugo katika maktaba ya baba yake. Alianza kutafsiri vitabu alivyovipenda zaidi kwenda katika lugha ya Kiarabu.[4]

Alipata shahada katika fasihi kutoka katika Chuo Kikuu cha Oran mwaka wa 1979, kabla ya kupata shahada yake ya uzamivu huko mjini Damascus mwaka 1990.[5]

Baada ya kuolewa na mwandishi Amin Zaoui, alifundisha katika Chuo Kikuu cha Oran hadi mwanzoni mwa miaka ya 1990. Kutokana na vitisho vya Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya nchini Algeria, wanandoa hao walihamia nchini Ufaransa mwaka wa 1995, na kurejea Algeria mwaka wa 2000.[6]

Baada ya kuanza kazi kama mwandishi wa habari, Djelti alianza kuandika mashairi kwa lugha ya Kiarabu mnamo mwaka wa 1981. Miongoni mwa diwani zake zilizofanikiwa zaidi ni Murmures du secret (mwaka wa 2002) na Qui est-ce dans le miroir (mwaka wa 2003), zilizotafsiriwa kwa Kifaransa na Abdellatif Laâbi na Rachid Boudjedra mtawalia.[7]

Mnamo Mwaka wa 2010 alianza kuandika riwaya, zikiwemo Le trône émaillé (mwaka wa 2013) na Nostalgie à la menthe (mwaka wa 2015).[8] Alieleza kuwa ingawa mashairi yake yalikuwa na hadithi ndani yake, alitamani kuandika riwaya kwa muda mrefu lakini alianza rasmi kufanya hivyo mwaka wa 2010.

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Djelti ameolewa na mwandishi wa nchini Algeria Amin Zaoui. Na mtoto wao wa kike,Lina Doran, ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo.[9]

  1. "SILA . Tour d'horizon des écrivains présents" (kwa Kifaransa). Elwatan. 2017-10-28. {{cite web}}: Missing or empty |url= (help)
  2. "Biographie De Rabia Djelti" (kwa Kifaransa). 2014-07-26. {{cite web}}: Missing or empty |url= (help)
  3. "3522.-Rabia Djelti" (kwa Kihispania). 2011-03-19. {{cite web}}: Missing or empty |url= (help)
  4. "Les vers voyageurs de Rabia Djelti". 2015-03-09. {{cite web}}: Missing or empty |url= (help)
  5. "Biographie De Rabia Djelti". {{cite web}}: Missing or empty |url= (help)
  6. "Biographie De Rabia Djelti". {{cite web}}: Missing or empty |url= (help)
  7. "Rabia Djelti présentera ses œuvres". 2016-04-10. {{cite web}}: Missing or empty |url= (help)
  8. "Rabia Djalti, poétesse romancière". 2016-04-19. {{cite web}}: Missing or empty |url= (help)
  9. "Lina Doran". {{cite web}}: Missing or empty |url= (help)
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rabia Djelti kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.