Nenda kwa yaliyomo

Pweza mwigaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
pweza mwigaji

Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Faila: Mollusca
Ngeli: Cephalopoda
Oda: Octopoda
Familia: Octopodidae
Jenasi: Thaumoctopus
Norman & Hochberg, 2005[1]
Spishi: T. mimicus
Norman & Hochberg, 2005[1]

Pweza mwigaji (Thaumoctopus mimicus) ni spishi ya pweza ya familia Octopodidae inayotokea katika Bahari ya Hindi na ya Pasifiki. Ana uwezo wa kuiga spishi nyingi nyingine za eneo hilo. Ni mashuhuri kwa kuwa na uwezo wa kubadilisha rangi ya ngozi yao na umbile asili ili kupatana na mazingira yao, kama vile mwamba uliofunikwa na mwani na matumbawe yaliyo karibu kupitia vifuko vya pigmenti vijulikanavyo kama chromatophores. Pweza mwigaji ana chromatophores na vile vile tabia ya pekee ya kuchukua sura ya vitu na wanyama mbalimbali. [2]

Pweza mwigaji ndiye mnyama pekee wa baharini ajulikanaye mpaka sasa mwenye kuweza kuiga aina mbalimbali za wanyama. Wanyama wengi wanaweza kuiga aina tofauti ili kuepuka au kuwatisha mahasimu, lakini pweza mwigaji pekee anaweza kuiga namna tofauti za maumbo ili kuepuka mahasimu.[3]

Asili na Ugunduzi

[hariri | hariri chanzo]

Pweza mwigaji kwanza aligunduliwa na kundi la wanasayansi mwaka 1998 mbali ya pwani ya Sulawesi, Indonesia. [4] Spishi hii ilidhaniwa hukaa tu Magharibi na kati ya Indo-Pasifiki (kwa wingi wa kumbukumbu zilizohifadhiwa kutoka Indonesia) hadi mmoja alipobainika karibu na mwamba mkubwa wa kizuizi kwenye kisiwa cha mjusi kilicho bapa na kina kifupi cha mchanga mnamo Juni 2012.[5]

Muonekano

[hariri | hariri chanzo]

Pweza mwigaji ni pweza mdogo, anayekua kufikia [urefu]] wa karibu sentimita 60 (futi 2), ikiwa ni pamoja na mikono, yenye kipenyo kinachokaribia penseli katika upana. Rangi ya asili ya pweza ni kahawia ang’avu/rangi ya mchanga, lakini kawaida huonekana na rangi liko zaidi ya mistari myeupe na kahawia kuwaogofya mahasimu kwa kuiga spishi zenye sumu na viumbe wa baharini wa matata wenye mipaka kwa maeneo yao. Uwezo wake wa kubadili umbo ndio sababu ya kupewa jina pweza "mwigaji", na ndio ulinzi wake mkuu licha ya kamafleji.

Tabia zilizochunguzwa

[hariri | hariri chanzo]

Anayeitwa "pweza mwigaji" wa kitropiki ya Indo-Pasifiki anafahamika kwa kuiga hadi aina 15 za viumbe wengine ndani ya bahari. Katika uigizaji wa mahali alipo, kuhangaika kwingi kulionekana; karibia matukio 500 yalichambuliwa. Spishi zote za pweza waliigiza umbo, uogeleaji, kasi, muda, na wakati mwingine mpangilio wa rangi wa utapatapaji wa kuogelea. Wakati wa uigaji kweta, pweza walisonga kikamilifu na wazi, ambapo mara moja kabla na baada ya hapo walikuwa wajifichao na wasiojongea (kukaa au kutambaa polepole). Aidha, wakati hawajongei, pweza wanatwaa ruwaza ya mwili na mkao fananishi na sponji ndogo, minyoo-mrija waliopo, au tunicates ya kikoloni, ambavyo vilikuwa miongoni mwa vitu vichache katika makazi mchanga wazi.

Ugunduzi muhimu ulikuwa kwa uigaji huo wa kweta pweza hutumia tu wakati wa harakati zake za kusogea kwamba unaweza kutoa kamafleji katika makazi haya yaliyo wazi. Katika visa vyote, pweza hutumia uigaji kama ulinzi wa msingi. Tabia ya kuiga ilibaki bila kugundulika kwa miaka kwa sababu mazingira yake yaliyofifia hayakuchunguzwa kwa ustadi. Lakini ni hasa katika mazingira haya tasa kwamba tabia hii ni faida. [6]

Pweza wanaweza kuiga wanyama wajulikanao kwa kuzuia mahasimu flani maalum wa kutisha. Kwa mfano imeonekana kwamba pweza anayeshambuliwa na damselfish humuigiza nyoka bahari milia wa nyeusi na njano, mhasimu wa damselfish. [7]

Sio tu pweza mwigaji huiga wanyama hawa tofauti, kutegemea na kiumbe gani anakumbana nae, pweza huiga viumbe tofauti. Anaamua tabia ya uigaji ambayo itakuwa sahihi zaidi na kuitekeleza.

Tabia za ulaji

[hariri | hariri chanzo]

Pweza mwigaji anaweza kuwekwa kama mwindaji au mtafutaji chakula wa kujitegemea. Anaaminika kuwa ni mwindaji kwa sababu wanasayansi waliona na kuandika kuwa pweza ana uwezo wa kunyemelea mawindo na kusaka samaki wadogo na kuwapata. Mara nyingi zaidi, hata hivyo, pweza mwigaji anaweza kuonekana kutafuta chakula kichakani. Anafanya hivyo kwa kutumia mchirizi wa ghafla wa maji kupitia neli yake kunyiririsha mchanga wakati wa kutafuta mawindo, na kutumia minyiri yake myembamba kufikia kwenye mashimo katika matumbawe, na pia mashimo kwenye mchanga, na kutumia vikombe vyake vya kunyonyea kunyakua krasteshia wadogo na kuwala. Kwa sababu pweza mwigaji anapendelea kuishi katika maji ya kina kifupi, maji ya utusiutusi, inaaminika kwamba mlo wake unakusanya karibu pekee ni samaki wadogo na krasteshia. Hiyo ni kwa sababu hao ni wanyama wawili tu ambao ni wa kawaida katika hali ya maeneo ambayo pweza mwigaji wanaweza kuishi. Wanaaminika kuwa ni walanyama, na hawajulikani kula aina yoyote ya mimea au uoto. [2] huishi katika bahari za kitropiki za Indo-Pasifiki, kwa mara ya kwanza aligundulika mwaka 1998 huko Sulawesi. [5][8] pweza huiga wanyama wengine kwa kutumia mabadiliko katika mpako wa rangi na Mkao wa mwili; kama cephalopods wengine pia ana uwezo wa kuiga usuli wake.

Pweza mwigaji ni tofauti na Wunderpus photogenicus, ambaye ana alama nyeupe zisizoondoka. [9] which has fixed white markings.[10]

Pweza mwigaji akionyesha ruwaza ya kawaida

Pweza mwigaji ni wa asili ya Indo-Pasifiki, kuanzia bahari ya Shamu katika nchi za Magharibi mpaka Kaledonia Mpya katika Mashariki, na Thailand na Ufilipino kaskazini hadi mwamba mkubwa wa kizuizi katika Kusini. [5][11] rekodi nyingi za kumbukumbu ni kutoka Indonesia. [5] hupatikana hasa katika maeneo yenye mchanga au mchangatope katika kina cha chini ya mita 15 (futi 49). [2] anapendelea sakafu ya bahari ya giza yenye tope ili kufanana na rangi yake asili kahawia, rangi ya mchanga.

  1. 1.0 1.1 Norman, M.D.; and Hochberg, F.G. (2005). "The 'mimic Octopus' (Thaumoctopus mimicus n. gen. et sp.), a new octopus from the tropical Indo-West Pacific (Cephalopoda: Octopodidae)." Molluscan Research 25: 57–70.
  2. 2.0 2.1 2.2 Maculay, G. (January 6, 2012). "Mimic Octopus Creature Feature - Diving with Mimics". Dive The World - Scuba Diving Vacations - Dive Travel - Diving Holidays - Liveaboards. Retrieved April 21, 2013.
  3. Harmon, K. (February 21, 2013). "Mimic Octopus Makes Home on Great Barrier Reef". Scientific American. Retrieved April 21, 2013.
  4. "Mimic Octopuses, Thaumoctopus mimicus". MarineBio. MarineBio Conservation Society. Januari 14, 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-10-25. Iliwekwa mnamo Desemba 17, 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. 5.0 5.1 5.2 5.3 Coker, Darren J. (2013). "Documentation of the mimic octopus Thaumoctopus mimicus in the Great Barrier Reef, Australia." Marine Biodiversity Records 1-2.
  6. Hanlon, R. T., Conroy, L.-A. and Forsythe, J. W. (2008), "Mimicry and foraging behaviour of two tropical sand-flat octopus species off North Sulawesi, Indonesia". Biological Journal of the Linnean Society, 93: 23–38. doi: 10.1111/j.1095-8312.2007.00948.x
  7. National Geographic: Newfound Octopus Impersonates Fish, Snakes. September 9, 2001.
  8. Piper, Ross (2007), Extraordinary Animals: An Encyclopedia of Curious and Unusual Animals, Greenwood Press. ISBN 978-0313339226
  9. Hochberg, F.G., M.D. Norman & J. Finn 2006. "Wunderpus photogenicus n. gen. and sp., a new octopus from the shallow waters of the Indo-Malayan Archipelago (Cephalopoda: Octopodidae)".PDF (805 KiB) Molluscan Research 26(3): 128–140.
  10. Norman, Mark (2000). Cephalopods: A World Guide. Hackenheim, Germany: ConchBooks. ku. 302–304. ISBN 3-925919-32-5.
  11. Nabhitabhata, Jaruwat; and Sukhsangchan, Charuay (2007). New Photographic Record of the Mimic Octopus in the Gulf of Thailand. Phuket Mar. Biol. Cent. Res. Bull. 68: 31–34.