Programufidia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Makala hiyo kuhusu "Programufidia" inatumia neno ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio kwa jambo linalotajwa.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.

Programufidia (kwa Kiingereza ransomware) ni aina ya programu haramu ambayo inakuzuia kutumia kompyuta yako hadi pale utakapolipa fidia kwa watu waliokutumia programu hiyo. Fidia mara nyingi hulipwa kwa kutumia sarafu dijitali kama vile Sarafu za Bit au Ukash.

Mashambulizi ya programufidia mara nyingi hufanyika kwa kutumia proramu ya Trojan ambayo inajifanya kuwa kama faili halali ambalo linamhadaa mtumiaji kompyuta kupakua au kufungua linapokuja kama kiambatanisho cha barua pepe. Hata hivyo, mfano mmoja wa teknolojia ya juu kabisa ya utapeli huu, "WannaCry worm", ilisafiri moja kwa moja kati ya kompyuta na kompyuta bila kuhitaji mtumiaji kufanya chochote.

Kuanzia mwaka wa 2012 matumizi ya programu hii yameongezeka kimataifa. [1] Kwa mfano, Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) linasema kuwa Programufidia aina ya CryptoWall ilivuna zaidi ya dola za Kimarekani milioni 18 hadi Juni 2015 kutokana na fidia za waathiriwa. [2]


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Kuenea kwa programufidia. Jalada kutoka ya awali juu ya 2014-07-02. Iliwekwa mnamo 2017-10-16.
  2. Ripoti ya FBI.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]