Priscillah Ruzibuka
Mandhari
Priscillah Umutashya Ruzibuka (alizaliwa 1991) ni mwanamke mjasiriamali kutoka nchini Rwanda ambaye ni mwanzilishi wa Ki-pepeo Kids Clothing, kampuni ya kijamii yenye lengo la kuwasaidia wanawake wasiojiweza.
Maisha ya Awali na Elimu
[hariri | hariri chanzo]Priscillah Ruzibuka alikuwa mtoto wa tatu kuzaliwa katika familia ya Wakatoliki. Alizaliwa Rwanda, lakini akiwa na umri mdogo yeye na familia yake walihamia nchi jirani, Tanzania. Baadaye walirudi Rwanda.
Ruzibuka ana Shahada ya Sayansi katika Uhandisi wa Teknolojia ya Habari kutoka Chuo Kikuu cha Multimedia nchini Malaysia na shahada ya uzamili katika usimamizi wa Miradi kutoka Chuo Kikuu cha Kikristo cha Oklahoma nchini Marekani. [1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Meet... PRISCILLA RUZIBUKA". theafrikanlegacy.com. 2017-06-07. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-05-03. Iliwekwa mnamo 2018-05-18.
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Priscillah Ruzibuka kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |