Nenda kwa yaliyomo

Princess Chitsulo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mizaya Princess Chitsulo (amezaliwa 1 Januari 1981), anayejulikana zaidi kama Princess Chitsulo, ni mwimbaji wa nyimbo za injili, na ni mwanaharakati na mfanyabiashara kutoka Malawi.[1][2] Mwaka 2001 alipokea tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kike katika shindano la Malawi Gin. Mwaka 2014 pia alitunukiwa tuzo ya Msanii Bora wa Kike, na wimbo wake Ndidzayimba Nyimbo (Nitaimba wimbo) ukachaguliwa kuwa Wimbo Bora wa Mwaka.[3]

Mwaka 2016, Chitsulo alishinda tuzo ya Msanii Bora wa Kike katika Magic Promotions, na mwaka 2018 alitunukiwa tuzo ya Msanii Bora wa Kike katika shughuli za kijamii.[2]

Chitsulo pia ni mwanzilishi wa shirika la misaada lijulikanalo kama Princess Chitsulo Foundation lililoanzishwa Desemba 2014 kwa lengo la kuwasaidia wazee, maskini na watoto walio katika mazingira magumu nchini Malawi.[4][5]

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Chitsulo alizaliwa tarehe 1 Januari 1981 katika wilaya ya Chiradzulu District nchini Malawi, akiwa mtoto wa mfanyabiashara na kiongozi wa jadi Raiden Chitsulo pamoja na Angellina Makatanje. Ana ndugu watatu ambao ni Tina, Margaret na Grace. Mama yake alifariki akiwa mdogo na hakuwa na kumbukumbu nyingi kumhusu. Akiwa na umri wa miaka 12, alipoteza baba yake. Baadaye yeye na ndugu zake walihamia kijijini kwao kabla ya kuhamia moja kwa moja mjini Blantyre kuishi na ndugu.

Alipata elimu ya sekondari katika shule za Chiradzulu Secondary School na Chichiri Secondary School. Pia alijiunga na kozi ya masoko katika Lehlonolo Business College lakini hakukamilisha kutokana na ukosefu wa msaada wa kifedha.

Matatizo ya kiafya
[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2000, Chitsulo aliugua ugonjwa wa meningitisi na kulazwa katika Queen Elizabeth Central Hospital. Mwaka 2014 aligundulika kuwa na tatizo la moyo na alipelekwa Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.[6] Marais wa zamani wa Malawi, Peter Mutharika na Joyce Banda, walitoa msaada wa kifedha ili aweze kusafiri kwa matibabu nchini Afrika Kusini.[7]

Kazi ya muziki

[hariri | hariri chanzo]

Chitsulo alianza kuimba mwanzoni mwa miaka ya 2000 na alitoa albamu yake ya kwanza mwaka 2000. Mwaka 2015 alitoa albamu yake ya pili iitwayo Mavutowa Akadzatha (Matatizo yatakapokwisha). Mwaka 2016 alitoa albamu yake ya tatu Nyimbo Yanga (Wimbo wangu) iliyokuwa na wimbo maarufu Chenjera Peturo (Kuwa mwangalifu Petro).[8][2] Mwaka 2023 alitoa albamu yake ya nne iitwayo Nsembe (Sadaka).[9]

Ameshirikiana na wasanii wa injili maarufu nchini humo kama Thoko Katimba na Ethel Kand pamoja na kwaya ya Great Angels Choir.[10]

Uanaharakati

[hariri | hariri chanzo]

Kupitia shirika lake la misaada, Chitsulo amekuwa akiwasaidia watu wenye ualbino nchini Malawi. Miongoni mwa misaada hiyo ni kutoa kiasi cha K24,000 kusaidia biashara ya ndizi kwa mtu mwenye ualbino aitwaye Constance Msiska huko Mzuzu.[4]

Mafanikio

[hariri | hariri chanzo]

Magic Promotions

[hariri | hariri chanzo]
Mwaka Mteule Kategoria Matokeo
2018 Yeye mwenyewe Best Gospel Act Alishinda

MUMA Awards

[hariri | hariri chanzo]

Chanzo:[3]

Mwaka Mteule Kategoria Matokeo
2014 Yeye mwenyewe Msanii Bora wa Kike Alishinda
2014 Ndidzayimba Nyimbo Wimbo Bora wa Mwaka Alishinda

Malawi Gin Competition

[hariri | hariri chanzo]
Mwaka Mteule Kategoria Matokeo
2001 Yeye mwenyewe Mwimbaji Bora wa Kike Alishinda

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Chitsulo alikuwa ameolewa na Albert Nyasulu ambaye alifariki miezi sita kabla ya kufanyika kwa harusi yao. Ana mtoto mmoja wa kike anayeitwa Sarah.

  1. ↑ Times, The Daily (2023-01-06). "Princess Chitsulo celebrates birthday with the needy". African News Agency (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-03-19.
  2. 1 2 3 "Princess Chitsulo album launch surpasses expectations: Ben Phiri supports cause with K0.5 mil - Malawi Nyasa Times - News from Malawi about Malawi". www.nyasatimes.com (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2016-10-03. Iliwekwa mnamo 2024-03-19.
  3. 1 2 MLOZI, HOWARD (2016-03-16). "2016 MUMA Awards to clear 2014 controversy | The Nation Online" (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-05-12. Iliwekwa mnamo 2024-03-19.
  4. 1 2 Loka, Chris (2016-11-01). "Person with albinism gets business boost from Princess Chitsulo Malawi 24 | Latest News from Malawi". Malawi 24 (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-03-19.
  5. ↑ "Princess Chitsulo Foundation pays tuition for 10 girls at South Lunzu CDSS - Malawi Nyasa Times - News from Malawi about Malawi". www.nyasatimes.com (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2018-04-27. Iliwekwa mnamo 2024-03-19.
  6. ↑ "Princes Chitsulo back: Fit and well - Malawi Nyasa Times - News from Malawi about Malawi". www.nyasatimes.com (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2014-05-27. Iliwekwa mnamo 2024-03-19.
  7. ↑ "JB, Mutharika assist gospel songstress Princess Chitsulo - Malawi Nyasa Times - News from Malawi about Malawi". www.nyasatimes.com (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2014-05-07. Iliwekwa mnamo 2024-03-19.
  8. ↑ https://allafrica.com/stories/201604080750.html. Iliwekwa mnamo 2024-03-19. {{cite web}}: Missing or empty |title= (help)
  9. ↑ Voice, Malawi (2023-02-21). "Gospel musician Princess Chitsulo set to release Nsembe album". Malawi Voice (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-03-19.
  10. ↑ "Namadingo, Chiwamba and Princess Chitsulo to share stage on Mother's day in Lilongwe - Malawi Nyasa Times - News from Malawi about Malawi". www.nyasatimes.com (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2018-09-24. Iliwekwa mnamo 2024-03-19.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Afrika bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Princess Chitsulo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.