Princella Adubea
Mandhari
Princella Adubea (alizaliwa tarehe 27 Desemba 1998) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa wanawake wa kitaalamu kutoka nchini Ghana anayekipiga kama mshambuliaji kwa klabu ya mpira ya Abu Dhabi Country Club nchini Emirati, pamoja na timu ya taifa ya wanawake ya Ghana.
Alimuwakilisha Ghana katika ngazi ya vijana chini ya umri wa miaka 20 katika Michuano ya Kombe la Dunia ya 2016 na 2018. Awali aliwahi kuchezea klabu ya Sporting de Huelva.[1][2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Adubea: Ghana striker joins Equatorial Guinea's Olanrewaju at Racing Santander | Goal.com". www.goal.com. Iliwekwa mnamo 2021-08-03.
- ↑ "Princella Adubea - Soccer player profile & career statistics - Global Sports Archive". globalsportsarchive.com. Iliwekwa mnamo 2021-08-03.
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Princella Adubea kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |