Nenda kwa yaliyomo

Porbandar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Porbander mwaka 2007
Hekalu ya Hanuman mjini Porbandar (1958)

Porbandar ni mji wa bandari kwenye pwani la Gujarat nchini Uhindi mwenye wakazi mnamo 150,000 (mwaka 2001). Inajulikana hasa kama mahali pa kuzaliwa kwa Mahatma Gandhi.

Jina la mji latokana na maneno mawili ya "Porai" ambayo ni jina la mungu wa kike anayeabudiwa hapa na "bandar" ambalo ni neno la Kiajemi la kumaanisha bandari.

Bandari iko kando la Bahari Hindi ni msingi kwa viwanda vya kushughulikia samaki inayopelekwa nje kutoka hapa.

Tangu karne ya 17 hadi uhuru wa Uhindi mji ulikuwa mji mkuu wa dola la maharaja wa Porbandar aliyetawala eneo la kilomita za mraba 1,663 na watu 100,000 chini ya usimamizi wa Uhindi wa Kiingereza.