Poractant Alfa
| Data ya kikliniki | |
|---|---|
| Majina ya kibiashara | Curosurf |
| AHFS/Drugs.com | Monograph |
| Kategoria ya ujauzito | N |
| Hali ya kisheria | ℞-only (US) |
| Njia mbalimbali za matumizi | Ndani ya njia ya hewa |
| Vitambulisho | |
| Nambari ya ATC | ? |
| Data ya kikemikali | |
| Fomyula | ? |
Poractant alfa, inayouzwa kwa jina la chapa Curosurf miongoni mwa nyinginezo, ni dawa inayotumika kutibu na kuzuia matatizo ya kupumua (RDS) kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.[1][2] Inapunguza hatari ya kifo na hali ya hewa kupenya kati ya utando wa mapafu na ukuta wa kifua (pneumothoraces).[2] Inatolewa kwenye trakea.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na mapigo ya moyo ya polepole, shinikizo la chini la damu na oksijeni ya chini.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha kuziba kwa mirija ya endotracheal.[1] Inajumuisha surfactant ya mapafu ambayo imeundwa na phospholipids na protini za surfactant.[1]
Dawa hii iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1999.[1] Nchini Marekani, iligharimu takriban dola 1,000 kwa mililita 3 kufikia mwaka wa 2021.[3] Dawa hii hutengenezwa kutoka kwa mapafu ya nguruwe.[1]
Marejeleo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 3 4 5 6 7 "Poractant Alfa Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 29 Oktoba 2021.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 "DailyMed - CUROSURF- poractant alfa suspension". dailymed.nlm.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 29 Oktoba 2021.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Curosurf Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 29 Oktoba 2021.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)