Pierrette Mari
Pierrette Mari (amezaliwa mwaka 1929) ni mtunzi wa muziki na mtaalamu wa taaluma ya muziki (*musicologist*) kutoka Ufaransa.
Maisha na kazi
[hariri | hariri chanzo]Pierrette Mari alizaliwa Nice na alisoma muziki katika Conservatory of Nice kuanzia mwaka 1943 hadi 1946. Aliingia Paris Conservatory mwaka 1950, ambapo alisoma chini ya Noël Gallon, Tony Aubin na Olivier Messiaen.
Alishinda tuzo ya kwanza katika counterpoint mwaka 1953 na tuzo ya kwanza katika fugue mwaka 1954. Mwaka 1956 alipata ufadhili wa masomo kuhudhuria Mkutano wa Muziki na Tamthilia huko Salzburg.[1]
Baada ya kukamilisha masomo yake, Mari aliandika kama mkosoaji wa muziki katika magazeti na majarida ya muziki. Pia alichapisha wasifu wa wanamuziki mashuhuri, wakiwemo Olivier Messiaen, Béla Bartók na Henri Dutilleux. Mwaka 1977 aliteuliwa kuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Paris, Sorbonne.[2]
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]- 1946: Tuzo ya Jiji la Nice
- 1961: Tuzo ya Kwanza katika wimbo wa Kifaransa (*French melody*), Umoja wa Kitaifa wa Sanaa
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Pierrette Mari kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |