Korogoto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Phyllastrephus)
Korogoto
Korogoto mkubwa
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Sylvioidea (Ndege kama kucha)
Familia: Pycnonotidae (Ndege walio na mnasaba na shore)
G.R. Gray, 1840
Ngazi za chini

Jenasi 3, spishi 27 za korogoto:

Korogoto ni ndege wadogo wa jenasi mbalimbali katika familia Pycnonotidae. Wanafanana na shore waliomo katika takriban kila bustani, lakini wana rangi ya zaituni juu na nyeupe, kijivu au njano chini. Nyembelele ni ndege wengine katika familia hii. Wanatokea misitu na maeneo mengine yenye miti katika Afrika kusini kwa Sahara. Hula matunda na mbegu hasa lakini wadudu pia. Tago lao hujengwa mtini na jike huyataga mayai 2-5.

Spishi[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]