Phylis Jepkemoi
Phylis Jepkemoi Bartoo ni mwanasiasa wa Kenya. Ni mwanachama wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) na mbunge wa jimbo la Moiben tangu mwaka 2022. Bartoo aliwahi kuwa mkuu wa kitivo cha sanaa na sayansi za kijamii katika Chuo Kikuu cha Egerton. Alisomea shahada ya kwanza ya Ualimu (B.EdArts) na shahada ya uzamili (master's) katika fani ya fiziolojia ya tiba katika Chuo Kikuu cha Kenyatta. Pia alisoma katika Chuo Kikuu cha Egerton Kenya ambapo alipata shahada ya uzamivu (MA) katika lugha na isimu. Zaidi ya hayo, alisoma katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand nchini Afrika Kusini, ambako alipata shahada ya uzamivu ya Ph.D. katika isimu. Kabla ya kuwa profesa mkuu katika isimu, alikuwa mwenyekiti wa Idara ya Fasihi, Lugha, na Isimu. Amekuwa profesa katika Chuo Kikuu cha Egerton kwa zaidi ya miaka kumi na tano.[1][2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Profile - DR PHYLIS JEPKEMOI BARTOO". www.egerton.ac.ke (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2023-03-23.
- ↑ "Keynote Speakers – KESSA" (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-06-16. Iliwekwa mnamo 2023-03-23.
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Phylis Jepkemoi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |