Nenda kwa yaliyomo

Phumzile Mlambo-Ngcuka

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Phumzile Mlambo-Ngcuka (alizaliwa 3 Novemba 1955)[1][2] ni mwanasiasa wa Afrika Kusini na mwakilishi wa zamani wa Umoja wa Mataifa, aliyehudumu kama Mkurugenzi Mtendaji wa UN Women akiwa na cheo cha Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Mlambo-Ngcuka alihudumu kama Makamu wa Rais wa Afrika Kusini kuanzia 2004 hadi 2008, akiwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo na wakati huo mwanamke mwenye cheo cha juu kabisa katika historia ya Afrika Kusini. Wakati akiwa makamu wa rais, alisimamia programu za kupambana na umasikini na kuhakikisha wanyonge wanapata faida kutokana na ukuaji wa uchumi.[3]

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Mlambo-Ngcuka alipata shahada ya kwanza (bachelor) katika sayansi ya jamii na elimu kutoka Chuo Kikuu cha Taifa cha Lesoth mwaka 1980, pamoja na shahada ya uzamili (master) katika filosofia kutoka Chuo Kikuu cha Cape Town mwaka 2003, iliyoangazia upangaji wa elimu na sera zake.[4] Mnamo 2013 alikamilisha udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Warwick. Kazi yake ilihusisha matumizi ya teknolojia ya simu kusaidia Maendeleo ya Walimu katika nchi zenye rasilimali chache. Alipokea udaktari heshima kutoka Chuo Kikuu cha Nelson Mandela Metropolitan mwaka 2014.

  1. "Profile". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-12-07. Iliwekwa mnamo 2025-09-18., South African Government Information.
  2. "SA history: Phumzile Mlambo-Ngcuka". sahistory.org. Iliwekwa mnamo 2021-03-20.
  3. "Phumzile Mlambo-Ngcuka". live.worldbank.org/experts/phumzile-mlambo-ngcuka.
  4. "cv" (PDF). www.unwomen.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2015-07-01. Iliwekwa mnamo 25 Agosti 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Phumzile Mlambo-Ngcuka kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.