Nenda kwa yaliyomo

Philomena Cheyech

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Philomena Cheyech Flomena Cheyech Daniel (alizaliwa Kaunti ya Pokot Magharibi, Kenya, 5 Julai 1982) ni mwanariadha wa Kenya anayeshindana katika mbio za mbali na marathon. Alipata rekodi yake binafsi ya 2:22:44 aliposhinda Paris Marathon 2014 na alikuwa mshindi wa medali ya dhahabu kwenye Michezo ya Madola 2014. Aliwakilisha Kenya kwenye IAAF Junior World Cross Country Championships 1999 huko Dublin, Eire, na kwenye IAAF World Half Marathon Championships 2009.

Alikaa Japani kati ya 2007 na 2010, akiendeshwa na timu ya kampuni ya Uniqlo, na alishinda Japanese Corporate Half Marathon mara mbili. Pia ameshinda marathon za Vienna na Toronto.[1]

  1. Gains, Paul (2013-10-20). Records galore at Toronto Marathon. IAAF. Retrieved on 2014-07-27.
Makala hii kuhusu mwanariadha wa Kenya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Philomena Cheyech kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.