Nenda kwa yaliyomo

Philippe Barbarin

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Philippe Barbarin

Philippe Xavier Christian Ignace Marie Barbarin (alizaliwa 17 Oktoba 1950) ni kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini Ufaransa ambaye alikuwa Askofu Mkuu wa Lyon kuanzia 2002 hadi 2020. Aliteuliwa kuwa kardinali mwaka 2003.

Mwaka 2017 alishtakiwa na mwaka 2019 alipatikana na hatia ya kushindwa kuripoti unyanyasaji wa kijinsia uliodaiwa kufanywa na kasisi mmoja akapewa adhabu ya kifungo cha miezi sita kilichosimamishwa.[1] Tarehe 24 Juni 2019, Barbarin aliacha uongozi wa Jimbo Kuu la Lyon, ingawa alibaki na cheo cha Askofu Mkuu. Hukumu hiyo ilibatilishwa kwa rufaa tarehe 30 Januari 2020, lakini Papa Fransisko alikubali kujiuzulu kwake kama Askofu Mkuu wa Lyon tarehe 6 Machi 2020.[2]

  1. "French court overturns earlier guilty verdict on cardinal Barbarin", Reuters, 30 January 2020. 
  2. Winfield, Nicole. "Pope lets French cardinal embroiled in abuse cover-up resign", Crux, 6 March 2020. 
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.