Nenda kwa yaliyomo

Philip Kiptoo Tunoi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Philip Kiptoo Tunoi ni wakili wa Kenya na Jaji mstaafu wa Mahakama ya Juu ya Kenya. Pia aliwahi kuhudumu kama Jaji wa Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki.

Jaji Tunoi ana shahada ya kwanza ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na shahada ya uzamili ya falsafa kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.[1] Alitunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) ya falsafa kutoka \[\[Chuo Kikuu cha Nairobi]] mwezi Desemba 2013.[2]

Jaji Tunoi alifanya kazi kama Wakili wa Serikali wa Mikoa ya Nyanza na Magharibi kuanzia mwaka 1970 hadi 1973 kabla ya kuingia katika mazoezi binafsi ya sheria hadi mwaka 1987. Alihudumu kama Jaji wa Mahakama Kuu ya Kenya kati ya mwaka 1987–1993 na baadaye kama Jaji wa Mahakama ya Rufaa ya Kenya kati ya mwaka 1993–2011. Jaji Tunoi pia ameshikilia nyadhifa mbalimbali ndani ya mahakama ya Kenya na Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki.[3][4]

  1. Hon. Justice P. K. Tunoi, Justice of the Supreme Court: http://kenyalaw.org/kl/index.php?id=3323
  2. The Hon. Justice Phillip Kiptoo Tunoi, Judge of the Supreme Court of Kenya, graduates with a PhD in the Philosophy of Law Ilihifadhiwa 21 Agosti 2017 kwenye Wayback Machine., Accessed 27 May 2014
  3. Judges Tunoi, Onyancha challenge retirement, Capital News, 27 May 2014. Accessed 29 May 2014
  4. Petition No. 244 of 2014, In the Matter Between Justice Philip K. Tunoi and Justice David A. Onyancha versus The Judicial Service Commission and The Judiciary, Ruling. Accessed 29 May 2014
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Philip Kiptoo Tunoi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.