Petro Juliani Eymard
Mandhari

Petro Juliani Eymard (La Mure, Grenoble, Ufaransa, 4 Februari 1811 – La Mure, 1 Agosti 1868) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki.
Kwanza mwanajimbo, baadaye alijiunga na Shirika la Maria na kutokana na imani yake kubwa kwa fumbo la ekaristi alianzisha mashirika mawili ya kitawa, moja la kiume na lingine la kike ili kuhamasisha na kueneza ibada kwa sakramenti hiyo kuu[1].
Alitangazwa mwenye heri na Papa Pius XI tarehe 12 Julai 1925, halafu mtakatifu na Papa Yohane XXIII tarehe 9 Desemba 1962. Papa Yohane Paulo II alimtangaza Eymard "Mtume wa Ekaristi".[2]
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/28550
- ↑ "Pelletier SSS, Norman B., "Peter Julian Eymard: The Apostle of the Eucharist", Emmanuel Magazine". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-11-06. Iliwekwa mnamo 2014-01-26.
- ↑ Martyrologium Romanum
Marejeo ya Kiswahili
[hariri | hariri chanzo]- John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 265-266
- Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 224-226
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Father Eymard's writing
- Letellier, Arthur. "Venerable Pierre-Julien Eymard." The Catholic Encyclopedia. Vol. 5. New York: Robert Appleton Company, 1909. 29 Jun. 2013
- Maisha yote na maisha ya kiroho ya Pierre-Julien Eymard kwa Kifaransa
- http://www.blessedsacrament.com/index2.html Ilihifadhiwa 16 Julai 2013 kwenye Wayback Machine. Tovuti ya Shirika la Sakramenti Takatifu
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |