Nenda kwa yaliyomo

Pete Seeger

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pete Seeger
Amezaliwa3, Mei 1919 Chelsea, Manhattan, New York, Marekani
Amekufa27, Januari 2014, (Miaka 94), New York, Marekani
Kazi yakeMwimbaji, mtunzi wa nyimbo, na mwanaharakati
Miaka ya kazi1939-2013
MtindoAmerican Folk Music, Muziki wa Kiharakati (Protest Music), Americana
MwenzaToshi Ohta (Kuoana 1943- kufariki 2013)
Saini

Peter Seeger (3 Mei 1919 – 27 Januari 2014) alikuwa mwimbaji, mwandishi wa nyimbo, mwanamuziki, na mwanaharakati wa kijamii wa Marekani. Alikuwa mtu mashuhuri kwenye redio za kitaifa mnamo miaka ya 1940, na alikuwa na mfululizo wa nyimbo zilizovuma sana (hit records) mwanzoni mwa miaka ya 1950 akiwa kama mwanachama wa kundi la The Weavers, hasa rekodi ya wimbo wa Lead Belly uitwao 'Goodnight, Irene', ambao ulikaa kileleni mwa chati za muziki kwa wiki 13 mnamo mwaka 1950.[1][2]

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Seeger alizaliwa tarehe 3 Mei 1919, katika Hospitali ya French huko Chelsea, Manhattan katika Jiji la New York. Familia yake, ambayo Seeger aliitaja kuwa 'ya Kikristo kupitiliza, katika tamaduni za Kipuritani na Kikalvini za New England', iliyobebwa na chimbuko la ukoo wake kwa zaidi ya miaka 200 nyuma. Babu wa upande wa baba, Karl Ludwig Seeger, tabibu kutoka Württemberg, Ujerumani, alihamia Amerika wakati wa Mapinduzi ya Marekani na kuoa katika familia ya zamani ya Parsons ya New England mnamo miaka ya 1780.[3][4]

Ingawa wazazi wa Peter walikuwa wanamuziki wa muziki wa kitambo (classical music), hawakumshinikiza kupiga chombo chochote cha muziki. Yeye mwenyewe, kijana ambaye kwa kawaida alikuwa mpenda vitabu na mpole wa kujitenga, alivutiwa na gitaa dogo la ukulele, akawa na ujuzi wa kuwaburudisha wanafunzi wenzake huku akiweka msingi wa uhusiano wake mzuri wa kushangaza na watazamaji hapo baadaye.[5][6][7]

  1. ↑ https://www.huffpost.com/entry/honor-pete-seeger_b_1883818
  2. ↑ https://www.latimes.com/entertainment/arts/culture/la-et-cm-pete-seeger-appreciation-20140209-story.html
  3. ↑ https://archive.org/details/charlesseegerlif00pesc/page/4/mode/2up
  4. ↑ https://digital.library.unt.edu/ark:/67531/metadc1692108/?q=Pete%20Seeger
  5. ↑ https://books.google.co.tz/books?id=xwLTDOR8LUYC&redir_esc=y
  6. ↑ https://www.newyorker.com/magazine/2006/04/17/the-protest-singer
  7. ↑ https://www.peggyseeger.com/ruth-crawford-seeger/ruth-crawford-seeger-biography
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pete Seeger kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.