Nenda kwa yaliyomo

Pekahia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfalme Pekahia alivyochorwa katika "Promptuarii Iconum Insigniorum" mwaka 1553.

Pekahia (kwa Kiebrania פְּקַחְיָה, Pəqaḥyā, yaani YHWH amefungua macho) alikuwa mwana wa Menahemu na mjukuu wa Gadi aliyepata kuwa mfalme wa Israeli miaka 2 (742 KK hivi - 740 KK hivi) baada ya baba yake kufa hadi alipouawa na Peka aliyeshika madaraka badala yake.

Biblia inamhukumu kwa kufuata sera ya kidini ya Yeroboamu I iliyowataka Waisraeli wamuabudu YHWH kwa sura ya fahali ya dhahabu katika mahekalu ya Dani na Beteli ili wasiende Yerusalemu, mji mkuu wa ufalme wa ukoo wa Daudi.

Habari zake zinapatikana hasa katika Kitabu cha Pili cha Wafalme 15:22-26.

    Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
    Je, unajua kitu kuhusu Pekahia kama habari za maisha au kazi yake?
    Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
    Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.