Nenda kwa yaliyomo

Peka

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfalme Peka alivyochorwa katika "Promptuarii Iconum Insigniorum" mwaka 1553.

Peka (kwa Kiebrania פֶּקַח, Peqaḥ) alikuwa kapteni wa mfalme Pekahia wa Israeli ambaye alimuua (740 KK hivi) akashika madaraka badala yake baada ya kuwa mpinzani wa mfalme Menahemu, baba wa Peka, tangu mwaka 752 KK[1][2][3][4]. Hatimaye mwaka 732 KK hivi aliuawa na Hoshea aliyeshika utawala kama mfalme wa mwisho wa Israeli.

Biblia inamhukumu Peka kwa kufuata sera ya kidini ya Yeroboamu I iliyowataka Waisraeli wamuabudu YHWH kwa sura ya fahali ya dhahabu katika mahekalu ya Dani na Beteli ili wasiende Yerusalemu, mji mkuu wa ufalme wa ukoo wa Daudi.

Habari zake zinapatikana hasa katika Kitabu cha Pili cha Wafalme 15:25-31.

  1. Cook, H. J., "Pekah," Vetus Testamentum 14 (1964) 14121–135.
  2. Carl Lederer, Die biblische Zeitrechnung vom Auszuge aus Ägypten bis zum Beginne der babylonischen Gefangenschaft, 1887, cited in Cook, Pekah 126, n. 1.
  3. Edwin R. Thiele, The Mysterious Numbers of the Hebrew Kings (3rd ed.; Grand Rapids, MI: Zondervan/Kregel, 1983) 129–134, 217.
  4. T. C. Mitchell, "Israel and Judah until the Revolt of Jehu (931–841 B.C.)" in Cambridge Ancient History 3, Part 1, ed. John Boardman et al. (Cambridge: Cambridge University Press, 1991) 326.
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Peka kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.