Nenda kwa yaliyomo

Paul Kelemba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pou kelemba

Amezaliwa 1962|6|25|
Nairobi, Kenya
Nchi Kenya

Paul Kelemba (alizaliwa Nairobi, 26 Juni 1962) ni msanii wa vibonzo vya katuni na mchoraji wa vikaragosi wa Kenya[1] aliyejifunza mwenyewe. Anatumia Maddo kama jina la kisanii, ambalo lilitokana na jarida la Mad Magazine la New York.

Baada ya kumaliza masomo yake, Paul Kelemba alianza kazi katika wakala wa matangazo wa hapa nchini mjini Mombasa, kisha baadaye akafanya kazi na majarida mbalimbali ya Kenya, yakiwemo Coastweek na Daily Nation, kama mchoraji wa vielelezo na katuni katika miaka ya 1980 na 1990.

Tangu mwaka 1992 Maddo amekuwa mwandishi wa ukurasa wa kejeli wa kila wiki unaoitwa It’s a Madd Madd World katika gazeti la The Standard (Kenya). Mwaka 2009 alikusanya kazi zake za It’s a Madd Madd World katika juzuu tatu wakati wa ukaaji wa mwezi mmoja katika Kituo cha Rockefeller Foundation Bellagio nchini Italia.

Umaarufu wake kimataifa unajumuisha ukaaji wa kisanii katika nchi za Japani, Estonia na Ujerumani.

Maddo ni mshindi wa Tuzo za CNN MultiChoice African Journalist Awards za mwaka 2015, ni mtayarishaji mshirika katika Buni Media Ltd, kampuni inayotayarisha kipindi cha The XYZ Show kilichopata msukumo kutoka kwa kipindi cha Kifaransa Les Guignols s,aidha yeye ni mwenyekiti wa Ketebul Music, shirika la majaribio ya aji wa muziki nchini Kenya linaloendeshwa na Tabu Osusa.[2][3]

  1. https://web.archive.org/web/20180503041642/http://bunimedia.com/portfolio/its-a-madd-madd-world/
  2. "It's a Madd Madd World101". Bunimedia. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-05-03. Iliwekwa mnamo 2018-05-02.
  3. "It's a Madd Madd World101". Bunimedia. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-05-03. Iliwekwa mnamo 2018-05-02.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Paul Kelemba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.