Pat Alger

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Pat Alger

Pat Alger (aliyezaliwa 23 Septemba 1947 Mjini LaGrange, Georgia[1]) ni mtunzi na mwimbaji wa Muziki wa Country na mchezaji Guitar.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Alger alihudhuria chuo cha Georgia Tech akisomea sanaa ya Ujenzi lakini akaamua kujishughulisha zaidi na kutunga nyimbo. Alianza kama mtumbuizaji wa nyimbo za kikale katika klabu. .[2]. Alianza kazi yake ya kutunga na kuimba nyimbo akishirikiana na Happy na Artie Traum kama mwanachama wa kundi la Woodstock Mountains Revue.Kundi hili lilishirikisha ndugu wa Trauma, John Herald na Maria Muldaur miongoni mwa wengine. Baadhi ya nyimbo alizozitunga wakati huu ni "Old Time Music" na "Southern Crescent Line."[1]. Mnamo 198o alikuwa na ufanisi wake wa kwanza kama mtunzi wakati when Livingston Taylor alikuwa na kibao kilichovuma kutoka "First Time Love". Kati ya 1984 na 1988 alizuru na Everly Brothers nchini Marekani na bara Uropa. .[2]. Baadaye alishirikiana na Nanci Griffith na wakaandika nyimbo za Griffith "Once In A Very Blue Moon" na "Lone Star State of Mind."[1]. Baadhi ya nyimbo zake pia zimefanya na by Kathy Mattea kama vile "Goin' Gone", "She Came From Fort Worth" na "A Few Good Things Remain." Aliandika baadhi ya hit #1 za Garth Brooks kama "Unanswered Prayers", "What She's Doing Now", "The Thunder Rolls" na "That Summer". Pia alitunga vibao kwa Hal Ketchum uitwao "Small Town Saturday Night," kwa Trisha Yearwood, "Like We Never Had A Broken Heart," kwa Don Williams, "True Love", na kwa Mark Collie, "Calloused Hands." Miaka hii yote, tunzi zake zimerekodiwa na kutolewa na wasanii wengi akiwemo Peter, Paul and Mary, Dolly Parton, Lyle Lovett, Brenda Lee na Crystal Gayle.[2] . Amerekodi albamu tatu za solo katika miiaka ya 1990 akishirikisha usaidizi kutoka kwa Griffith, Lovett, Mattea na Yearwood.[3].

Amekuwa ha ngoma zaidi ya 20 ambazo zimevuma zikiwemo nane katika chati ya ‘’Number One Hits’’. Alikuwa nyota katika rizala za 30 za Washington Center for the Performing Arts gala. mPia alishirikishwa katika kipindi cha redio ya NPR "All Things Considered".

Tuzo[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 1991 alituzwa kama Mtunzi wa Mwaka na Nashville Songwriter's Association International, na mwaka huo huo akatuzwa kwa kuwa Mtunzi wa Jukebox wa mwaka na shirika la American Society of Composers, Authors and Publishers, ASCAP.

Mnamo 1992, alipata tuzo la Mtunzi wa nyimbo za Country wa mwaka na ASCAP. Country Music Association ilimpa tuzo mbili za Triple Play ambalo hupewa wasanii walio na hit #1 tatu kwa mwaka.[4]

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Alger mara ya kwanza alitayarisha albamu iliyokuwa ikimshirikisha msanii Artie Traum hatimaye akatoa albamu zingine tatu za solo:

  • From The Heart (1980)
  • True Love & Other Short Stories - Sugar Hill Records (1991)
  • Seeds - Sugar Hill Records (1993)
  • Notes and Grace Notes (1994)

Vidokezo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 Carlin 2003, p. 3.
  2. 2.0 2.1 2.2 Miller 1996, p. 9.
  3. Miller 1996, p. 10.
  4. Miller 1996, p. 11.

Virejeleo[hariri | hariri chanzo]

  • Carlin, Richard (2003), Country Music: A Biograhical Dictionary, Taylor & Francis
  • Miller, Zell (1996), They Heard Georgia Singing, Mercer University Press