Pascal Joy Migisha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Pascal Joy Migisha (alizaliwa Buyenzi-Bujumbura, Burundi, 25 Aprili, 1972) ni Mwinjilisti wa Kipentekoste.

Alizaliwa mara ya pili katika umri wa miaka 14 mwaka 1986 katika Shule la Msingi. Pascal Joy Migisha alijiunga na chuo cha Biblia Emmaus cha Morsbach Ujerumani ambapo alifanya utafiti wake Biblia kwa njia ya mawasiliano 1994-2002.

Baada ya uongozi wa Kanisa nchini Zimbabwe mwaka 2002, aliondoka Zimbabwe na kuelekea Afrika Kusini ambapo alifanya miaka miwili ya masomo ya ziada ya Biblia katika Chuo Kikuu cha Cape Town chini ya Taasisi ya Every Nation Leadership Institute, baada ya hapo aliwezeshwa kuendelea katika uongozi wa Shirika la Kikristo alilolianzisha mwenyewe Julai 1995, Evangelism and Reconciliation for all Nations (“ERNA”).

Mpaka sasa, misingi ya Shririka la ERNA ipo katika nchi ya Burundi (mashariki / kati ya Afrika) na huduma zaidi zinaendeshwa Afrika Kusini, katika kufikia au kuwahubiri vijana katika shule, makanisa, na mikutano ya Injili katika jamii, bila kusahau misaada kwa watu wote walio katika mazingira magumu Burundi na Afrika Kusini. Tayari Pascal Joy Migisha ametoa ushuhuda wake kwa mamia ya maelfu ya vijana wa Burundi, DRC, Tanzania, Malawi, Zimbabwe na hasa Afrika Kusini ambapo anawahubiri vijana kwa wingi katika shule za msingi na za sekondari. Hadi sasa, ameongoza mamia ya maelfu ya vijana na wazee kwa Kristo. Anaendelea kuhubiri Kristo kwa wote, bila kujali rangi, kabila, utaifa, umri, mila, hali ya kijamii... Yeye anasema hashindani na mtu yeyote, hataki kumvutia mtu yeyote, hana haja ya kutafuta heshima na utukufu kwa wanadamu. Bali anafanya kila kitu kwa ajili ya utukufu wa Mungu, jinsi Yeye anavyomuongoza.

Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pascal Joy Migisha kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.