Nenda kwa yaliyomo

Parashqevi Qiriazi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Parashqevi Qiriazi

Parashqevi Qiriazi (anajulikana kama Paraskevi D. Kyrias; 1886 - 1970) alikuwa mwalimu, mkurugenzi wa shule, na mchapishaji kutoka nchi ya Albania, ambaye alijitolea maisha yake kuendeleza elimu kwa lugha ya  Kialbania iliyoandikwa. Alikuwa mshiriki katika Kongamano la Manastir mwaka 1908, ambalo liliamua herufi za alfabeti ya kisasa ya kialbania, na alikuwa mmoja wa wajumbe wanawake wachache waliotumwa kuwakilisha taifa lake katika mkutano wa amani wa Paris mwaka 1919.

Parashqevi alizaliwa Monastir, katika Manastir Vilayet, milki ya Ottoman ambayo ni Makedonia Kaskazini ya leo.[1] Alipokuwa na umri wa miaka 11 tu alianza kumsaidia kaka yake Gjerasim Qiriazi na dada yake Sevasti Qiriazi kuwafundisha wasichana Kialbania kwa maandishi katika shule ya kwanza ya wasichana huko Albania, iitwayo shule ya wasichana (kwa lugha ya Kialbania: Shkolla e Vashave), ambayo ilifunguliwa mwezi oktoba 1891.[1][2]

Baadaye alikwenda Marekani na kuwa mwanachama wa jumuiya ya waalbania-wamarekani, ambapo alishiriki katika mkutano wa amani wa Paris mwaka 1919 ili kuwakilisha haki za Waalbania.[3][4]

Parashqevi alisimama imara kama mpinga ufashisti katika vita vya pili vya dunia, kuanzia uvamizi wa Italia mwaka 1939. Kwa sababu ya msimamo wake wa kupinga ufashisti, yeye pamoja na dada yake walipelekwa kwenye kambi ya Anhaltelager Dedinje karibu na Belgrade na vikosi vinavyounga mkono Nazi vilivyoongozwa na Xhaferr Deva.[5][6]

  1. 1 2 Elsie, Robert (2001). A Dictionary of Albanian Religion, Mythology, and Folk Culture (kwa Kiingereza). NYU Press. ISBN 978-0-8147-2214-5.
  2. Haan, Francisca de; Daskalova, Krasimira; Loutfi, Anna (2006-01-01). Biographical Dictionary of Women's Movements and Feminisms in Central, Eastern, and South Eastern Europe: 19th and 20th Centuries (kwa Kiingereza). Central European University Press. ISBN 978-963-7326-39-4.
  3. Sharp, Ingrid; Stibbe, Matthew (2011-02-14). Aftermaths of War: Women's Movements and Female Activists, 1918-1923 (kwa Kiingereza). BRILL. ISBN 978-90-04-19172-3.
  4. "Parashqevi Qiriazi, e vetmja grua e Kongresit të Manastirit". www.kolonja.com (kwa Kiingereza (Uingereza)). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-03-24. Iliwekwa mnamo 2026-02-17.
  5. "Kosova Sot", Kosova Sot (kwa Kiingereza), ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-09-27, iliwekwa mnamo 2026-02-17
  6. "Familja atdhetare Qiriazi dhe mjeshtri i madh i turpit (T.B.)", PrishtinaPress.info (kwa American English), iliwekwa mnamo 2026-02-17