Papa Paulo I

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Papa Paul I)
Mt. Paulo I.

Papa Paulo I alikuwa Papa kuanzia mwezi Aprili au tarehe 29 Mei 757 hadi kifo chake tarehe 28 Juni 767[1]. Alitokea Roma, Lazio, Italia[2] katika familia Orsini[3] [4].

Alimfuata Papa Stefano II ambaye alikuwa kaka yake, akafuatwa na Papa Stefano III.

Kabla ya kuteuliwa Papa alikuwa shemasi na kutumwa na kaka yake kupatana na Walombardi waliotawala sehemu kubwa ya Italia. Alichaguliwa ili kuendeleza sera hiyo, naye alijitahidi kutetea haki za Kanisa kwa msaada wa mfalme wa Wafaranki, Pipino Mfupi, ingawa kwa kufanya hivyo alimchukiza kaisari wa Dola la Roma Mashariki[5].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa kwenye tarehe ya kifo chake[6].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  2. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  3. McClintock, John; Strong, James (April 15, 1882). Cyclopaedia of Biblical, Theological, and Ecclesiastical Literature VII. Harper. uk. 831 – kutoka Internet Archive. Pope Paul I.  Check date values in: |date= (help)
  4. George L. Williams, Papal Genealogy (London 2004).
  5. https://www.santiebeati.it/dettaglio/89093
  6. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Paulo I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.