Nenda kwa yaliyomo

Pablo Escobar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pablo Escobar (1976)

Pablo Escobar (1 Desemba 19492 Desemba 1993) alikuwa mfanyabiashara wa madawa ya kulevya kutoka Kolombia huko Marekani.

Kijana huyu, kipindi yupo darasa la saba, alikuwa anawaambia wenzake kwamba atakapomaliza darasa la saba atashika dola za Kimarekani bilioni 30. Alipomaliza darasa la saba alianza kutimiza ndoto yake kwa kuuza madawa ya kulevya huko Kolombia. Mpaka mwaka 1980 alikuwa msafirishaji mkubwa wa cocaine. Pia alipata kuwa mmoja wa matajiri duniani kwa muda mfupi.

Mwaka 1991 alijisalimisha kwa maafisa wa polisi kwa makosa mengi ikampelekea kufungwa miaka mitano jela. Alichaguliwa kukaa gereza lake mwenyewe. Alitoroka mwaka 1992 akiwa anapelekwa kituo kidogo cha kawaida cha kushikilia, na kusababisha msako wa kitaifa. Mnamo mwaka 1993 aliuwawa na polisi wa taifa la Kolombia.

Alifariki akiwa na miaka 44.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pablo Escobar kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.