Kisaidizi binafsi cha kidijitali

Kisaidizi binafsi cha kidijitali (Kiingereza: Personal digital assistant; kifupi PDA) ni kifaa kidogo cha mkononi chenye matumizi mengi, ambacho hutumika kusaidia kupanga taarifa binafsi. Baada ya kuwa maarufu sana miaka ya 1990 na 2000, PDA nyingi zilianza kupoteza umaarufu baada ya watu wengi kuanza kutumia simujaja zenye uwezo mkubwa zaidi, hasa zile zinazotumia iOS na Android mwishoni mwa miaka ya 2000, na kwa hiyo matumizi yake yakapungua kwa haraka.[1][2]
PDA huwa na skrini ya kuonyesha vitu kwa njia ya kielektroniki. Aina nyingi pia huwa na uwezo wa kutoa sauti, hivyo zinaweza kutumika kama kicheza media kidogo (kifaa cha kubeba na kucheza sauti/video), na zingine pia kama simu. Kufikia mwanzo wa miaka ya 2000, karibu kila PDA ilikuwa na uwezo wa kuunganishwa na Intaneti, intranets au extranets kwa kutumia Wi-Fi au WAN, zisizo na waya. Pia nyingi zikawa na kivinjari cha simu. Baadhi ya PDA za baadaye zilitumia kioo cha kupapasa badala ya vitufe.
Historia
[hariri | hariri chanzo]
PDA ya kwanza kabisa iliitwa Organiser, na ilitolewa mwaka 1984 na kampuni ya Psion. Kisha ikafuata Psion Series 3 mwaka 1991, ambayo ilianza kufanana na PDA tunazozifahamu, ikiwa na kibodi kamili.[3][4] Neno PDA lilitumiwa kwa mara ya kwanza tarehe 7 Januari 1992 na Mkurugenzi Mkuu wa Apple Inc., John Sculley, katika maonesho ya Consumer Electronics Show huko Las Vegas, Nevada, akimaanisha Apple Newton.[5]

Mwaka 1994, IBM ilitoa PDA ya kwanza yenye uwezo wa kutumia simu ya analojia, iitwayo IBM Simon, ambayo pia inaweza kuchukuliwa kama simujanja ya kwanza. Kisha mwaka 1996, Nokia ilitoa PDA yenye simu ya kidigitali, iitwayo 9000 Communicator.
Kampuni nyingine iliyokuwa ya kwanza katika soko hili ni Palm, ambayo ilianza kuuza mfululizo wa bidhaa za PDA mwezi Machi 1996.[6] Palm ilikuja kutawala soko la PDAs hadi zilipoanza kushindanishwa na vifaa vya Pocket PC mwanzoni mwa miaka ya 2000.[7]
Kufikia katikati ya miaka ya 2000, karibu kila PDA ilianza kuwa simujanja, kwa kuwa zile ambazo hazikuwa na uwezo wa kupiga simu zilianza kupotea sokoni.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Andrew Smith, Faithe Wempen (2011). CompTIA Strata Study Guide. John Wiley & Sons. uk. 140. ISBN 978-0-470-97742-2. Iliwekwa mnamo 5 Julai 2012.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Edwards, Benj (Novemba 20, 2018). "The Golden Age of PDAs". PC Magazine. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Septemba 24, 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "The Protea Story". The Register. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Julai 2013. Iliwekwa mnamo 10 Agosti 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Litchfield, Steve (1998). "The History of Psion". Palmtop Magazine. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Julai 22, 2011. Iliwekwa mnamo 9 Juni 2015 – kutoka Clove Technology.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Newton, Reconsidered – Time magazine, 1 June 2012
- ↑ Krazit, Tom (Machi 27, 2006). "Ten years on, revisiting Palm's first Pilot". Zdnet. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Aprili 9, 2025.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Kane, Margaret (Januari 31, 2002). "Palm's market position erodes". Cnet. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Agosti 10, 2022.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |