Ousmane Dembele

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ousmane Dembele

Ousmane Dembélé (alizaliwa 15 Mei 1997) ni mchezaji wa soka wa Ufaransa ambaye anachezea klabu ya Barcelona F.C. na timu ya kitaifa ya Ufaransa.

Dembélé alianza kazi yake ya soka huko Rennes kabla ya kujiunga na klabu ya Dortmund mwaka 2016. Mwaka mmoja baadaye, alihamia Barcelona kwa ada ya awali ya milioni 105.

Borussia Dortmund[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kushinda Vikombe 20 na kufunga magoli matano katika ngazi ya vijana, Dembélé alipandishwa kwenda ligi daraja la kwanza mwaka 2016 na klabu ya Borussia Dortmund.

Mnamo Mei 12, 2016, Dembélé alisaini mkataba wa miaka mitano na klabu ya Ujerumani Borussia Dortmund. Mnamo tarehe 14 Agosti 2016, Dembélé alianza kucheza na kushinda 2-0 dhidi ya Bayern Munich katika DFL-Supercup.

FC Barcelona[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 25 Agosti 2017, FC Barcelona ya La Liga ilitangaza kuwa wamefikia makubaliano ya kutia saini kwamba wanataka kumnunua Dembélé kwa € milioni 105 pamoja na kuongeza milioni 40 za ziada.

Ousman dembele alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na Barcelona dhidi ya Espanyol ambapo aliotokea benchi na kutoa assisting kwa Luis Suarez Barcelona wakishindi 4-0. Alicheza tena mechi yake ya pili dhidi ya Juventus katika klabu bingwa Ulaya. Mechi yake ya tatu ilikuwa dhidi ya Granada ambapo aliumia na kukaa nje kwa myezi minne.

Alirudi Desemba 2017 kwenye mechi dhidi ya Celta Vigo kwenye kombe la mfalme.

Bao lake la kwanza alifunga dhidi ya Chelsea kwenye ligi ya mabingwa Ulaya. Bao lake la kwanza kwenye La Liga alifunga dhidi ya Celta Vigo kwenye sare ya 2-2.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ousmane Dembele kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.