Nenda kwa yaliyomo

Taya (mnyama)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ourebia ourebi)
Taya
Dume la Taya (Ourebia ourebi)
Dume la Taya
(Ourebia ourebi)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyana wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Artiodactyla (Wanyama wenye vidole viwili au vinne mguuni)
Nusuoda: Ruminantia (Wanyama wanaocheua)
Familia: Bovidae (Wanyama walio na mnasaba na ng'ombe)
J. E. Gray, 1821
Nusufamilia: Antilopinae (Wanyama wanaofanana na swala)
Jenasi: Ourebia (Taya)
Laurillard, 1842
Spishi: O. ourebi
Zimmermann, 1782
Msambao wa taya
Msambao wa taya

Taya, kasia au vihea (Ourebia ourebi) ni swala wadogo wenye miguu myembamba na shingo ndefu ambao wanatokea savana za Afrika kusini kwa Sahara.

Taya wazima wana urefu wa sm 92–110, kimo cha sm 50–66 begani na uzito wa kg 12–22. Wanaweza kukimbia kwa mbio wa km 40–50 kwa saa. Wakifugwa huishi hadi miaka 14.

Mgongo na kidari cha juu ni njano hadi kahawiamachungwa. Kidevu, koo, kidari cha chini na tumbo ni nyeupe na kuna mviringo mweupe kwa matako. Mkia ni mfupi na una manyoya mengi; upande wa juu ni mweusi au kahawianyeusi na upande wa chini ni mweupe. Baka jeupe kwa umbo wa hilali juu ya jicho ni hulka inayosaidia kutofautiana spishi hii na swala wengine wanaoonekana hivyo hivyo. Mianzi ya pua ni myekundu na chini ya masikio liko baka jeusi kubwa la mviringo lililo na tezi. Tezi nyingine ziko pande za uso ambazo zinatoa uto ulio na kidusi na unaotumika kwa kutopoa bara la taya. Dume tu ana pembe ambazo ni nyembamba na wima na zina nyushi kwa nusu ya chini; nusu ya juu ni laini na ina ncha kali. Urefu wa pembe ni hadi sm 19.

Msambao na makazi

[hariri | hariri chanzo]

Taya wanatokea takriban nchi zote za Afrika kusini kwa Sahara. Usambazaji unaenda kutoka Senegali mpaka Uhabeshi ya magharibi na ya kati na Somalia ya kusini, kuendelea upande wa kusini katika Kenya na Uganda mpaka Botswana ya kaskazini na Angola. Katika Msumbiji, Zimbabwe na sehemu za kati na mashariki za Afrika Kusini usambazaji wao ni kirakaraka na si mzima.

Kwa kawaida Taya hukaa katika mbuga wazi au maeneo ya kichaka kisicho kizito. Hupenda maeneo ya manyasi mafupi ambayo wanayala, lakini yenye manyasi marefu pia ambayo ndani yao hujifichia wanyama mbua. Taya hutegemea maji sana na huepuka miteremko ishukayo sana.

Wakati wa majira ya kuzaa, kutoka Agosti hadi Desemba, dume hupanda majike wote wanaogawana bara lake naye. Kwa kawaida majike mmoja au wawili tu wamo katika kila bara. Baada ya muda wa mimba wa miezi 6–7 mtoto mmoja azaliwa. Pindi ya wiki 8–10 za kwanza jike huficha mwanake katika manyasi mazito ambapo atalala bila kujongea akikaribiwa. Mamake hurudi mara kwa mara kumnyonyesha. Watoto hulikizwa baada ya miezi 4–5. Majike hupevua baada ya miezi 10, madume baada ya miezi 14.

Jike la taya

Taya wanahitari kula manyasi mafupi lakini hula majani na machipukizi wakati wa kiangazi. Huonekana mara nyingi katika maeneo yaliyochomeka wakila machipukizi mapya ya manyasi. Ili kuongezea mlo wao hulamba chumvi ya asili.

Taya wana maadui wengi, k.m. simba, chui, simbamangu, fisi, mbwa mwitu, bweha, mamba na chatu. Watoto hukamatwa pia na tai, kanu na wanyama mbua wadogo wengine.

Mwenendo

[hariri | hariri chanzo]

Taya huishi peke yao, kwa jozi au kwa makundi ya dume mmoja pamoja na majike mawili au zaidi. Hupumzika wakati wa joto la mchana na hufanya amali yao asubuhi, alasiri na jioni. Wakishtuka hupiga mbinja ikwaruzayo. Mara nyingi hawajaribu kukimbia lakini hukaa bila kujongea kati ya manyasi hadi adui amekuja katika mita chache wakitegemea kamafleji. Endapo wanatishwa huondoka shoti wakiruka kwa miguu ishupaayo kila nyago kadhaa (hiyo huitwa stotting kwa Kiingereza).

Maafa na hifadhi

[hariri | hariri chanzo]
Taya nchini Niger

Idadi za taya zinakamwa na tenzi za watu kama:

  • Uharibifu wa makazi – Mbuga zinapotea kwa sababu ya nyongeza ya makao, kupanda kwa kibiashara kwa miti, kilimo cha kibiashara, udhalili wa mbuga na ng'ombe wengi sana, moto, mmomonyoko na uchimbaji.
  • Mawindo yasiyoruhusiwa, k.m. kutega wanyama kwa matanzi. Mawindo ya taya kwa mbwa ni afa kubwa yaliyopunguza idadi za taya katika Afrika Kusini.

Kwa bahati nzuri taya wanatokea hifadhi nyingi. Pia hufugwa ili kuachiliwa katika makazi yanayowafalia.

Nususpishi

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]

Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.