Nenda kwa yaliyomo

Oswald Gracias

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Oswald Gracias

Oswald Gracias (alizaliwa 24 Desemba 1944) ni mtaalamu wa Kanisa Katoliki kutoka India ambaye amekuwa Askofu Mkuu wa Bombay tangu mwaka 2006. Aliteuliwa kuwa kardinali mwaka 2007. Mnamo mwaka 2008, alikua makamu rais wa Mkutano wa Maaskofu Katoliki wa India. Mwaka 2010, alichaguliwa kuwa rais.

Gracias alikuwa rais wa Shirikisho la Mikutano ya Maaskofu wa Asia kutoka 2010 hadi 2019. Mnamo mwaka 2013, aliteuliwa kuwa mwanachama wa Baraza la Makardinali, lililoanzishwa na Papa Fransisko kumsaidia katika mageuzi ya utawala wa kati wa Kanisa Katoliki. Gracias alizingatiwa kuwa mmoja wa watakaoweza kuwa Papa mwaka 2013. [1]

  1. (in it) Rinunce e Nomine, 28.09.2000 (Press release). Holy See Press Office. 28 September 2000. https://press.vatican.va/content/salastampa/it/bollettino/pubblico/2000/09/28/0565/01954.html. Retrieved 3 February 2020.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.