Nenda kwa yaliyomo

Oscar Kikoyo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Dkt. Oscar Ishengoma Kikoyo (alizaliwa 22 Februari 1970) ni mtaalamu wa sheria na mdau wa elimu, pia mwanasiasa wa Tanzania katika chama cha CCM na sasa ni Mbunge wa jimbo la Muleba Kusini tangu 2020. [1]

Mwaka 2001 alifunga ndoa na Dkt. Levina Apolinary Kikoyo (Mkurugenzi mstaafu wa Pact nchini Tanzania), na kujaliwa nae watoto wanne; Cuthbert Kikoyo, Carlin Kikoyo, Cassian Kikoyo na Carson Kikoyo.

Mwanasiasa

[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2020, kama mwana chama cha CCM mwenye haki zote za kugombea na kupigiwa kura halali aliamua kuwania kiti cha ubunge jimbo lake la Muleba Kusini na kupata ushindi wa kura 90,610 sawa na asilimia 70 mwaka huo huo 2020 na kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa awamu ya kwanza.

Mwaka 2025 aligombea tena nafasi ya ubunge jimbo la Muleba Kusini kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo kwa awamu ya pili kupitia chama chake; Chama cha Mapinduzi na kushinda kwa kura 167, 291 sawa na asilimia 97.6 ya kura halali zilizopigwa kwenye jimbo hilo na kuendelea kuwa mbunge wa jimbo hilo.

  1. Tovuti ya Bunge la Tanzania Ilihifadhiwa 11 Juni 2017 kwenye Wayback Machine., iliangaliwa Januari 2020
Makala hii kuhusu kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Oscar Kikoyo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.