Oscar Kambona
Oscar Salathiel Kambona (13 Agosti 1928 – 3 Juni 1997)[1] [2]alikuwa Waziri wa Kwanza wa Mambo ya Nje wa Tanganyika kuanzia mwaka 1963 hadi 1966.
Alikuwa mwana wa mchungaji David Kambona na Miriam Kambona. Baba yake alikuwa miongoni mwa wachungaji wa kwanza Waafrika waliopadrishwa katika Kanisa la Anglikana Tanganyika. Kambona alipata elimu yake ya msingi nyumbani, akifundishwa na wazazi wake pamoja na mjomba wake, wote wakiwa ni walimu. Baadaye alitumwa kusoma katika Shule ya Kati ya Mtakatifu Barnaba (St. Barnabas Middle School) huko Liuli, Kusini mwa Tanganyika, karibu na nyumbani kwao. Kisha aliendelea na masomo yake katika Shule ya Sekondari ya Alliance iliyopo Dodoma, katikati mwa Tanganyika.
Kazi ya Kisiasa
[hariri | hariri chanzo]Kambona aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha TANU (Tanganyika African National Union) wakati wa harakati za kudai uhuru, na alifanya kazi kwa ukaribu na Julius Nyerere, ambaye alikuwa Rais wa TANU, chama kilichoongoza Tanganyika kupata uhuru. Tanganyika ilipata uhuru kutoka kwa Uingereza tarehe 9 Desemba 1961.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu kuhusu mwanasiasa wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Oscar Kambona kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |