Nenda kwa yaliyomo

Orodha ya nchi za Afrika ya Mashariki kwa Pato la Taifa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Pato la taifa la Afrika ya Mashariki ni takriban dola bilioni 511 za Marekani ikiwa ni asilimia 17.98% ya uchumi wa Afrika.Kenya ndiyo iliyo na pato la taifa kubwa zaidi katika Afrika ya Mashariki ikiwa na asilimia 26% ya jumla ya uchumi wa Afrika Mashariki ikiwa na takriban dola bilioni 131 za Marekani, Ethiopia na Tanzania zina pato la taifa la bilioni 117 na 85 mtawaliwa. Shelisheli na Komori ndizo zilizokuwa na pato la taifa chache sana.[1]

OrodhaNchiPLTAsilimia ya Jumla
-Afrika Mashariki511.96100.00%
1 Kenya131.6725.72%
2 Ethiopia117.4622.94%
3 Tanzania85.9816.79%
4 Uganda64.2812.56%
5 Sudan31.516.15%
6 Madagaska18.713.65%
7 Morisi15.53.03%
8 Rwanda14.772.88%
9 Somalia12.992.54%
10 Burundi6.751.32%
11 Jibuti4.590.90%
12 Sudan Kusini40.78%
13 Shelisheli2.20.43%
14 Komori1.550.30%

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "East Africa by gdp" (kwa Kiingereza). 2025. Iliwekwa mnamo 2025-04-22.