Nenda kwa yaliyomo

Orodha ya nchi kwa Kiashiria cha Maendeleo ya Binadamu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwa mwaka wa 2024, Isilandi ilikuwa na Kielelezo cha Maendeleo ya Binadamu (HDI) cha juu zaidi duniani kwa alama ya 0.972, ikifuatiwa na Norwei (0.970), Uswisi (0.967) na Udeni] (0.962). Kwa upande mwingine, Sudan Kusini ilikuwa na HDI ya chini kabisa duniani kwa alama ya 0.388, ikifuatiwa na Somalia (0.404) na Jamhuri ya Afrika ya Kati (0.414). Wastani wa HDI ulikuwa juu zaidi katika Ulaya ya Magharibi, huku Afrika ya Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiorodheshwa kuwa na wastani wa chini zaidi. Nchi iliyoongoza kwa ukuaji mkubwa wa HDI ilikuwa Nauru, kwa ongezeko la 1.84%, ikifuatiwa na Haiti (1.74%) na Eswatini (1.70%).

Orodha

[hariri | hariri chanzo]

Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu inajumuisha takwimu kwa mataifa yote 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa,[1] pamoja na Hong Kong na Palestina. [2] Kwa jumla, HDI inapatikana kwa mataifa 192 na eneo moja. [3]

  1. Nations, United. "Member States" (kwa Kiingereza). United Nations. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Juni 2022. Iliwekwa mnamo 2023-04-06.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "A World Tour of the States not recognized by the UN". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Desemba 2022. Iliwekwa mnamo 6 Desemba 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Human Development Report 2025 - A matter of choice: People and possibilities in the age of AI. United Nations Development Programme. 6 Mei 2025. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Mei 2025. Iliwekwa mnamo 6 Mei 2025.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  1. HDI not available before 2011 in latest report
  2. HDI not available before 2022
  3. HDI not available before 2022