Orodha ya Vyuo Vikuu vya Ufini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nchini Ufini taasisi za elimu ya juu zimeteuliwa na sheria (Yliopistolaki, 645/1997).[1] Kulingana na amri kuhusu mfumo wa shahada katika taasisi za elimu ya juu (Asetus korkeakoulututkintojen järjestelmästä 464/1998), vyuo vikuu katika kitengo cha alempi korkeakoulututkinto (shahada ya kwanza) na ylempi korkeakoulututkinto (shahada ya uzamili) na shahada ya uzamifu.[2]

Kando na vyuo vikuu, nchi ya Ufini ina mifumo mingine ya taasisi za elimu ya juu zinazoitwa ammattikorkeakoulu, ambazo hutafsiriwa kama vyuo vya ufundi anwai ama vyuo vikuu vya matumizi ya sayansi. Tasisi hizi zimeorodheshwa katika makala haya kama vyuo vya ufundi nchini Ufini. Taasisi za elimu za ammattikorkeakoulus zina uhuru wa kutoza shahada katika vitengo vya ammattikorkeakoulututkinto na ylempi ammattikorkeakoulututkinto. Katika matumizi ya kimataifa shahada hizi huainishwa kama shahada za kwanza na uzamili.[3]

Vyuo Vikuu[hariri | hariri chanzo]

Vyuo vikuu vya Ufini (Vimeainishwa kwa mujibu wa miaka ya uanzilishi)

Chuo kikuu cha Ulinzi wa Kitaifa hakitambuliwi kama Chuo Kikuu katika sheria za Ufini, ingawaje kimeidhinishwa kutoza shahada za kwanza, uzamili na uzamifu na kufanya utafiti. Athari za tofauti hizi ni chache mno, zinatambulika tu katika uteuzi wa wasimamizi wa chuo hicho kikuu, kinachoongozwa na wanajeshi badala ya raia. Hata hivyo, chuo hiki kimeorodheswa hapa kwa sababu mkuu ya chuo ni mwnachama wa Baraza la Wakuu wa Vyuo Ufini.[4]

Vyeo vya vyuo kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Kulingana na Orodha ya QS ya Ubora wa Vyuo Vikuu Duniani:

Taasisi 2004 2005 2006 2007 2008 2009
Chuo kikuu cha Helsinki (Helsingin yliopisto) 129 62 116 100 91 108
Chuo kikuu cha teknolojia cha Helsinki (Teknillinen korkeakoulu) 176 194 NR 170 NR NR

NR = hakuna uorodheshaji baada ya 200 bora.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Yliopistolaki (645/1997). Archived 27 Novemba 2009 at the Wayback Machine. 1 §. Rudishwa 10-3-2007. (Kifini)
  2. http://www.finlex.fi/fi/laki/alkup/1998/19980464 Archived 14 Mei 2011 at the Wayback Machine. Asetus korkeakoulututkintojen järjestelmästä (464/1998) kama amri iliyopita na 426/2005] 1.1 §, sehemu ya 1 na 8 §. Rudishwa 10-3-2007. (Kifini)
  3. http://www.finlex.fi/fi/laki/alkup/1998/19980464 Archived 14 Mei 2011 at the Wayback Machine. Asetus korkeakoulututkintojen järjestelmästä (464/1998) kama amri iliyopita na 426/2005] 1.1 §, sehemu ya 3 na 10 §. Rudishwa 10-3-2007. (Kifini)
  4. Suomen yliopistojen rehtorien neuvosto. Archived 17 Februari 2009 at the Wayback Machine.Jäsenyliopistot. Archived 17 Februari 2009 at the Wayback Machine. Rudishwa 10-3-2007.