Orodha ya Messier

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Orodha ya Messier (tamka mes-ye; Messier Catalogue) ni orodha ya nyota iliyotungwa na mwanaastronomia Mfaransa Charles Messier kati ya 1764 na 1782.

Messier alitafuta hasa nyotamkia angani akitumia darubini. Aliona pia magimba mengine yaliyoonekana kama nebula (wingu dogo linalong'aa) zisizotembea angani kwa hiyo hazikuwa nyotamkia. Akaamua kuziorodhesha.

Orodha hii ilikuwa orodha ya kwanza iliyokubaliwa na wanaastronomia wengi kimataifa. Nyota na nebula zake zilijulikana kufuatana na namba jinsi zilivyoandikwa katika orodha ya Messier yaani M1, M2 na kadhalika. M1 ni Nebula ya Kaa, M45 ni fungunyota ya Kilimia na galaksi ya Andromeda ni M31.

Kuna namba 110 katika orodha hii.

Orodha za nyota za kisasa zinaonyesha nyota malakhi lakini namba za Messier zinaendelea kutumiwa hadi leo kwa vitu vinavyoorodhesha kwake.