Orciprenaline
| Jina la (IUPAC) | |
|---|---|
| (RS)-5-[1-hydroxy-2-(isopropylamino)ethyl]benzene-1,3-diol | |
| Data ya kikliniki | |
| Majina ya kibiashara | Alupent, mengineyo |
| AHFS/Drugs.com | Monograph |
| MedlinePlus | a682084 |
| Kategoria ya ujauzito | A(AU) C(US) |
| Hali ya kisheria | Prescription Only (S4) (AU) ℞-only (US) |
| Njia mbalimbali za matumizi | Kuvuta pumzi (MDI) and vidonge |
| Data ya utendakazi | |
| Uingiaji katika mzunguko wa mwili | 3% kwa kuvuta pumzi, 40% kwa njia ya mdomo |
| Kimetaboliki | Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na ini |
| Nusu uhai | Masaa 6 |
| Vitambulisho | |
| Nambari ya ATC | ? |
| Data ya kikemikali | |
| Fomyula | C11H17NO3 |
| |
| Data ya kimwili | |
| Umumunyifu katika maji | 9.7 mg/mL (20 °C) |
| | |
Orciprenaline, pia inajulikana kama metaproterenol, ni dawa inayotumika kutibu pumu (asthma) na ugonjwa sugu wa kupumua (COPD).[1] Inachukuliwa kwa mdomo au kwa kuvuta pumzi.[1] Dawa za salbutamol au terbutaline zinapendekezwa kwa kuwa zina ufanisi zaidi na athari mbaya kidogo.[2]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na wasiwasi, mtetemeko, maumivu ya kichwa, mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida (palpitations), matatizo ya kulala, kuhara na kuhisi kuwashwa.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha potasiamu ya chini na kubanwa kwa njia za hewa (bronchospasm).[1] Ni kichocheo cha kipokezi cha adrenergiki vya β2 (β2 adrenergic receptor agonist) ambacho hulegeza misuli laini kwenye njia za hewa.[1]
Orciprenaline iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1973.[1] Nchini Marekani, vidonge 90 vya miligramu 20 viligharimu takriban dola za Kimarekani 54 kufikia mwaka 2021.[3] Dawa hii iliondolewa kwenye soko nchini Uingereza mwaka wa 2010.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 3 4 5 6 "Metaproterenol Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 25 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 16 Novemba 2021.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - 1 2 "Orciprenaline sulphate (Alupent): reminder of withdrawal from the market". GOV.UK (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Julai 2017. Iliwekwa mnamo 17 Novemba 2021.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Metaproterenol Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo 17 Novemba 2021.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)