Orchestra Mambo Bado

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Orchestra Mambo Bado
Picha ya Assossa iliyotoka kwenye tangazo la kwanza la bendi, hapa akiwa amevaa shati la ndege ambalo kwa siku hizo walikuwa wanavaa wajanja tu.
Picha ya Assossa iliyotoka kwenye tangazo la kwanza la bendi, hapa akiwa amevaa shati la ndege ambalo kwa siku hizo walikuwa wanavaa wajanja tu.
Maelezo ya awali
Asili yake Dar es Salaam, Tanzania
Aina ya muziki Muziki wa dansi
Miaka ya kazi 1983/83 - 1985

Orchestra Mambo Bado ilikuwa bendi ya muziki wa dansi kutoka Dar es Salaam, Tanzania. Bendi ilianzishwa na mnamo 1982/83 ikiwa chini ya Tchimanga Kalala Assossa, kwa bahati mbaya, bendi haikudumu sana ikafa.

Historia yake[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1982/83 Tchimanga Kalala Assossa alianzisha na kuongoza bendi iliyoweza kutia changa moto katika ulimwengu wa muziki wakati huo. Bendi hiyo iliitwa Orchestra Mambo Bado na mtindo wake wa Bomoa Tutajenga Kesho. Wanamuziki katika bendi hiyo walikuwa Tchimanga Assossa, Kiongozi na mwimbaji, Kazembe wa Kazembe mpiga solo (pamoja na jina hilo alikuwa Msukuma), William Maselenge, rythm guitar, Huluka Uvuruge solo gitaa ya pili, Sadi Mnala drums, Mzee Albert Milonge solo ya pili, Lucas Faustin mwimbaji, John Kitime muimbaji na rythm guitar, George Mzee muimbaji, Athuman Cholilo muimbaji, Likisi Matola Bass na keyboards, Jenipher Ndesile mwimbaji, Selemani Nyanga Drums. Albamu ya kwanza ya bendi hii ilikuwa na nyimbo zilizotamba kama vile Kutokuelewana, Bomoa Tutajenga Kesho , hii ilipigwa marufuku.

Mwanzo zama za DDC Mlimani Park hadi Mambo Bado[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1981 Bendi ya DDC Mlimani Park ilimfuata Kongo na kumleta tena hapa nchini ambapo mkataba wake ulipomalizika alirudi Kongo tena kwao akiwa kaacha kibao kinachokwenda kwa jina la ‘Gama Unisamehe’. Mwaka uliofuata alifuatwa tena na Mzee Makassy, na kukaa na bendi ya Orchestra Makassy na hatimaye mwaka 1984 kutua kwenye kundi la Orchestra Mambo Bado alipokutana na nyota kadhaa.

Miongoni mwa nyota hao ni mwanadada Jenifa Ndesire, John Kitime, Likisi Matola, William Maselenge, Huluka Uvuruge, Sadi Mnala, George Mzee pamoja na Lucas Faustine ambaye kwa mara ya mwisho alikuwa Polisi Brass Band. Nyota yake ya kimuziki ilianza kung'aa vyema akiwa Orchestra Mambo Bado, kwani aliibuka na vibao vingi moto wa kuoteambali, kama vile; ‘Bomoa Tutajenga Kesho’ na Kutokuelewana, Chance na vinginevyo”. Alidumu Mambo Bado kwa muda mfupi tu kwani mwaka 1985 alirudi tena Maquis Original, bendi iliyokuwa imekusanya magwiji wengi wa muziki wa dansi kuliko zote nchini Tanzania.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]