Nenda kwa yaliyomo

Operesheni Dudula

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Operesheni Dudula ni harakati iliyoanzishwa nchini South Africa ambayo baadaye ilijigeuzwa kuwa chama cha siasa. Kundi hilo limekuwa likijulikana kwa kampeni zake zinazolenga kupinga uhamiaji na kuwafukuza wahamiaji wanaoishi nchini humo.[1]

Jina "Dudula" ni neno la Kizulu lenye maana ya "kuwafukuza" au "kuwaondoa", likionyesha lengo kuu la harakati hiyo la kuondoa wahamiaji wanaodaiwa kuishi au kufanya kazi nchini Afrika Kusini kinyume cha sheria.[2]

Operation Dudula ilianzishwa katika mji wa Soweto, karibu na mji mkuu wa Afrik Kusini, Johannesburg, na baadaye ikaenea katika maeneo mengine ya nchi. Kundi hilo linadai kuwa changamoto nyingi za kijamii na kiuchumi nchini Afrika Kusini zinachangiwa na uhamiaji haramu, usimamizi dhaifu wa mipaka, na sera za uhamiaji zisizo kali.[3][4]

Hata hivyo, harakati hiyo imekumbwa na ukosoaji mkubwa kutoka kwa wanaharakati wa haki za binadamu, mashirika ya kiraia na baadhi ya viongozi wa kisiasa, ambao wameituhumu kwa kuchochea chuki dhidi ya wageni (xenophobia) na kuhusishwa na vitisho au mashambulizi dhidi ya wahamiaji. Kwa upande wake, Operation Dudula imekuwa ikikanusha kuwa harakati zake zinachochewa na chuki dhidi ya wageni.

Kiongozi wa sasa wa kundi hilo ni Zandile Dabula.

  1. Operation Dudula has brought fascism to South Africa, Imraan Buccus, Sunday Times, 3 August 2025
  2. Charlie, Ayanda; Ford, Tamasin (17 Septemba 2023). "Inside South Africa's Operation Dudula: 'Why we hate foreigners'". BBC News.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Myeni, Thabi. "What is Operation Dudula, South Africa's anti-migration vigilante?". www.aljazeera.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-04-10.
  4. Ho, Ufrieda (2022-04-16). "XENOPHOBIA: Nhlanhla Lux exposed – The disturbing picture behind the masks of the man heading Operation Dudula". Daily Maverick (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-05-04.
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Operesheni Dudula Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.