Ono

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 21:20, 9 Machi 2013 na Addbot (majadiliano | michango) (Bot: Migrating 27 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q335046 (translate me))

Ono ni hali inayompata binadamu au mnyama kwa ndani, lakini inajitokeza kwa nje (inaonekana).

Ni tofauti na hali ya makusudi, kwa kuwa linasababishwa na jambo fulani.

Ndiyo maana katika Kiingereza linaitwa passion, neno la mkopo kutoka lile la Kilatini passio linalotokana na kitenzi patior (kupatwa).

Maono ni mbalimbali, lakini yale ya msingi ni: upande mmoja pendo (kwa jambo fulani), linalosababisha hamu (ya jambo hilo) na hatimaye furaha (jambo likipatikana); upande mwingine chuki (kwa jambo fulani), linalosababisha hofu (ya jambo hofu), hasira (dhidi ya hilo) na hatimaye huzuni (jambo likipatikana).