Omoyemi Akerele

Omoyemi Akerele (alizaliwa Lagos, Nigeria, 13 Mei 1978) ni mfanyabiashara na mjasiriamali wa nchini Nigeria [1], mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa tamasha la Lagos Fashion Week.
Maisha ya awali na kazi
[hariri | hariri chanzo]Akerele alipata Shahada ya awali katika sheria kutoka Chuo Kikuu cha Lagos na Shahada ya uzamili katika sheria ya kiuchumi wa Kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Warwick. Kuanzia 2000 hadi 2003, alifanya kazi katika kampuni ya wanasheria ya Nigeria ya Olaniwun Ajayi & Co.
Mnamo 2004, aliacha tasnia ya sheria ili kuelekeza juhudi zake katika kuanzisha na kukuza tasnia ya mitindo ya nguo za Nigeria. Baadae, alianzisha kampuni ya ushauri ya Exclusive Styling akiwa na Bola Balogun, na walitengeneza mitindo ya watu mashuhuri kwa vipindi vya televisheni vikiwemo Big Brother, Idols West Africa na Deal or No Deal. Akerele alikuwa mhariri wa mitindo kutoka 2005 hadi 2010 wa jarida la mitindo, urembo na mtindo wa maisha la wanawake weusi True Love.[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Momentum. Lagos Fashion and Design Week". system-magazine.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-07-22.
- ↑ Okoroafor, Thia (2015-10-27). "Interview: As LFDW 2015 begins, Omoyemi Akerele talks about the future of fashion on the continent". Ventures Africa (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-07-22.