Nenda kwa yaliyomo

Olubukola Mary Akinpelu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Olubukola Mary Akinpelu (alimaarufu Mylifeasugar) ni muuguzi aliyesajiliwa kutoka nchi ya Nigeria mwenye asili ya Marekani, mwalimu wa muuguzi, na muundaji wa maudhui. Yeye ndiye mwandishi wa Mwongozo wa Utafiti wa Shule ya Uuguzi ya Ultimate .

Alifanikiwa kupata tuzo ya Vitabu vya Rekodi vya Nigeria,na tuzo nyingine aliyoipata ni ile Tuzo ya Hisani ya JOM na nyingine pia ni Tuzo za Yessiey kutokana na michango yake kwenye taaluma ya afya na uuguzi.

Olubukola anatoka eneo la Lagelu LGA, Ibadan, Jimbo la Oyo nchini Nigeria. Alielimishwa masomo ya shule ya msingi katika East Gate, masomo ya sekondari katika Chuo cha Wasichana cha Serikali ya Shirikisho, Oyo na masomo ya chuoni kwenye Chuo cha Jumuiya cha Houston kabla ya kupata Shahada yake ya Sayansi kwenye Uuguzi (BSN) ndani ya Chuo Kikuu cha Lamar huko jijini Texas, Marekani, na kupata Shahada ya Kwanza ya Sayansi. Alihamisha makazi Marekani ili aweze kuendelea na elimu yake, akipata vigezo vya muuguzi aliyepitishwa kutoka Bodi ya Uuguzi ya Texas.

Olubukola alikuwa ni mwanzilishi wa elimu ya utunzaji wa wauguzi na mfumo wa kutoa huduma ka jamii za vijijini. Alifanya jukumu la msingi kwenye kupunguza ueneaji wa magonjwa na kuweka ubora kwenye huduma ya afya kwa ujumla nchini Nigeria na alitoa mchango kwenye maendeleo ya programu za elimu nchi ya Nigeria kwa watu na jamii duni kwa kuwapa elimu juu ya desturi za usafi.

Pia alisimamia ongezeko la upatikanaji wa elimu ya uuguzi na kupinga kabisa ubaguzi wa ndani ya taaluma hiyo. Wakati cha janga la COVID-19, alitengeneza taarifa ya maswala ya afya yenye lengo juu ya uuguzi na pia alichukua la msingi juu ya huduma ya afya ya Nigeria kwa kuwapa mafunzo wauguzi bure kipindi cha amri iliyotoka nje ili kuunga mkono serikali kwenye kupunguza kusambaa kwa virusi hivyo.

Kwa kutumia njia ya Nadharia yake ya Mahitaji pamoja na elimu ya juu ya uuguzi na utafiti kwa kusimamia mradi wa kuelezea fasihi ya uuguzi, alitoa msaada kwenye kuunda uuguzi nchini Nigeria.

Anafahamika katikati ya mwa wauguzi watatu bora wa nchini Nigeria na mwalimu wa kwanza wa wauguzi kwenye jamii yake ya karibu na mwaka wa 2023, aliandikwa na Jarida la Yessiey amekuwa kati ya watu 100 wenye nguvu wa kushawishi watu kwenye bara la Afrika.

Tuzo na utambuzi

[hariri | hariri chanzo]

Mwaka wa 2021, Vitabu vya Rekodi vya Nigeria vilimheshimisha kwa mafanikio yake, mwaka wa 2022 na mwaka wa 2023 alitunukiwa Tuzo ya Hisani ya JOM na Tuzo za Yessiey mtawalia.

Aliandikwa kati ya watu 100 wenye ushawishi mkubwa ndani ya bara la Afrika na kupewa heshima miongoni mwa watoa elimu watatu bora wa wauguzi wa Nigeria.