Olubankole Wellington

Olubankole Wellington (maarufu kwa jina lake la kisanii Banky W anatajwa katika filamu kama Banky Wellington; amezaliwa Marekani, 27 Machi 1981) ni mwimbaji, rapa, mwigizaji, mjasiriamali na mwanasiasa mwenye asili ya Nigeria.[1][2][3][4]
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Familia yake ilirejea Nigeria alipokuwa na umri wa miaka mitano. Alianza kuimba akiwa mdogo katika kwaya ya kanisa lao. Kabila lake ni la Wayoruba.[5]
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Wellington alipata elimu yake ya msingi jijini Lagos, Nigeria. Baadaye alisoma katika Shule ya Sekondari ya Home Science Association kwa elimu ya sekondari. Kisha alirejea kuendeleza masomo yake ya juu katika chuo cha Rensselaer Polytechnic Institute, New York, Marekani, kwa ufadhili wa masomo. Akiwa chuoni, mnamo mwaka 2002, alianzisha lebo ya muziki ya Empire Mates Entertainment (E.M.E). Pia aliwahi kufanya kazi katika GlobalSpec.
Mnamo mwaka 2009, aliondoka Marekani na kurejea Nigeria, ambako alianzisha rasmi lebo yake ya muziki jijini Lagos kwa kuwasaini wasanii kama Niyola, Shaydee, Skales, na Wizkid. Mnamo mwaka 2005, alitoa albamu yake ya kwanza ya studio iitwayo Back in the Building.[6] Wimbo wake wa kwanza ulikuwa Ebute Metta.[7]
Wellington pia ndiye aliyeandika wimbo wa kwanza wa matangazo wa kampuni ya simu ya Etisalat Nigeria ulioitwa "0809ja for Life".
Albamu na Rekodi
[hariri | hariri chanzo]Albamu za studio
- Back in the Building (2006)
- Mr. Capable (2008)
- The W Experience (2009)
- R&BW (2013)
- Songs About U (2017)
- The Bank Statements (2021)
EPs
- Undeniable (2003)
Albamu za mkusanyiko
- Empire Mates State of Mind (2012)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Yoruba, NG Movies. "Meet Actor/Actress Banky W | Movies by Banky W". NG Movies Yoruba (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-07-31.
- ↑ "Banky Wellington: 'Music was a platform to get in the door'". BBC News.
- ↑ "Banky Wellington Archives".
- ↑ "Without sounding arrogant, I'm confident of defeating Banky W – Obanikoro". Punch Newspapers (kwa American English). 2022-07-07. Iliwekwa mnamo 2022-07-17.
- ↑ Okonofua, Odion (2017-11-27). "10 mambo usiyoyajua kuhusu wanandoa maarufu". Pulse Nigeria (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-07-31.
- ↑ Jane Aguoye (9 Desemba 2017). "INTERVIEW: My wife and our new movie — Banky W". Premium Times. Iliwekwa mnamo 30 Desemba 2017.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Banky W faces criticisms on Ebute Metta". Vanguard. 2 Desemba 2011.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Olubankole Wellington kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |