Oktava
Mandhari
(Elekezwa kutoka Oktava ya Pasaka)
Oktava (kutoka Kilatini: octava (dies), yaani (siku) ya nane) ni ya mwisho katika mfululizo za siku nane za kusherehekea fumbo muhimu la wokovu katika liturujia ya Kikristo, hasa Noeli na Pasaka, lakini zamani Epifania, Pentekoste na sikukuu nyingine pia. Jina hilo linatumika vilevile kwa siku zote nane pamoja [1].
Chanzo cha desturi hiyo ni Yesu mfufuka kuwatokea tena wanafunzi wake siku ya nane baada ya Pasaka yake (Yoh 20:26), hivi kwamba Wakristo walianza kuadhimisha Dominika kila siku ya nane [2][3].
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Oxford Dictionary of the Christian Church (Oxford University Press 2005 ISBN 978-0-19-280290-3), article Octave
- ↑ Irénée Henri Dalmais, Pierre Jounel, Aimé Georges Martimort, The Liturgy and Time (Liturgical Press 1986 ISBN 978-0-81461366-5), p. 18
- ↑ Kenneth A. Strand, The Sabbath In Scripture (Review and Herald Pub Assoc 1982 ISBN 978-0-82802094-7), p. 143
| Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Oktava kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |