Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Mandhari
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa | |
---|---|
Mamlaka | Tanzania |
Makao Makuu | Dodoma City centre |
Waziri | Selemani Said Jafo |
Tovuti | tamisemi.go.tz |
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ni wizara kamili ambayo ipo chini ya Ofisi ya Rais na kusimamiwa na Waziri wa nchi akisaidiwa na manaibu wawili wao kama wasimamizi. Pia kuna Katibu mkuu ambaye yeye ni mtendaji Mkuu wa kila siku wa shughuli za serikali.
Mojawapo ya kazi za Wizara hii ni kuratibu mipango yote ya maendeleo ya mikoa pamoja na Serikali za Mitaa chini ya uangalizi wa ofisi ya Rais. Dhamana ya uendeshaji wa Wizara hii upo chini ya Waziri ambaye pia ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Tanzania.
Wizara hii imebeba dhamana ya maendeleo ya kimaeneo katika Mikoa na mitaa yake yote, hasa katika kuhakikisha kwamba miundombinu ya kila eneo kwenye ujenzi wa barabara na majumba inaendelea, tena kwa kiwango kilichostahili.
Marejeo
Tazama pia
Viungo vya nje
- Tovuti Archived 17 Juni 2018 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |